Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Masele

Spika Ndugai ataja kosa kubwa analoshtakiwa Masele

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele, hawezi kukaidi tena agizo la kutakiwa kufika Kamati ya Maadili baada ya kuitwa na Spika huyo kwa mara ya pili. Spika wa Bunge Job Ndugai. Akizungumza na waandishi wa habari Spika Ndugai amesema suala la Bunge kumuita Masele halihusiani na matukio yaliyotokea Afrika Kusini bali ni kwa sababu ya mambo aliyofanya nyumbani. Spika Ndugai amesema " ameitwa kwa mambo ya hapa nyumbani ya utovu wa nidhamu, anaunganisha hilo na matendo anayoyafanya huko, lakini hatujamuita kwa mambo ya South Afrika Watanzania watulie baada ya muda zitaletwa bungeni kila mtu atasikia kuhusu anatuhumiwa nini na majibu yake yalikuwa nini na wataelewa kama ameonewa au hajaonewa ." " Stephen Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda sababu awe mkimbizi na  akirudi Tanzania lazima aje Kamati ya Maadili, ni wito wa kisheria tunachomuitia ni tabia yake uchonganishi wa viongozi, kwa sasa hatu...

Masele: Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya

Natii wito wa Ndugai, nataka kujua mambo ya hovyo hovyo nayoyafanya- Masele Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP), Steven Masele amesema kuwa ameamua kuitikia wito wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ili kuweza kujua ni mambo gani ya hovyo hovyo anayoyafanya. Ameyasema hayo wakati akizungumza na DW ambapo amedai kuwa yeye alikuwa akitimiza majukumu yake ya kuongoza kamati maalum ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili rais wa bunge la Afrika, Nkodo Dang. Amesema kuwa anarejea nyumbani Tanzania ili kuitikia wito huo na kutaka yawekwe wazi kwa wananchi hayo mambo ya hovyo hovyo anayoyafanya huko Afrika Kusini sehemu ambayo ni kituo chake cha kazi. ”Nimemsikiliza Spika wangu Job Ndugai sijamuelewa, niko njiani narudi nyumbani Tanzania kuweza kujua hayo mabo ya hovyo hovyo ninayoyafanya ni yapi, na pale nilikuwa natekeleza majuk...