Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya REKODI

Israel: Isaak Hayik avunja rekodi ya mchezaji soka mkongwe zaidi duniani

Haak Hayik mchezaji soka mkongwe duniani Mchezaji wa soka wa Israel, Isaak Hayik aliye na miaka 73 amevunja rekodi ya kuwa mwanasoka mkongwe zaidi duniani. Isaak aliandikisha historia hiyo baada ya kucheza kama mlinda lango wa timu ya Israeli ya Ironi ama Yehuda siku ya Ijumaa. Licha ya umri wake mkubwa, Hayik alisema "yuko tayari kwa mchezo mwingine" baada ya kucheza kwa dakika 90. Amepokea tuzo ya Guinness World Records katika hafla iliyoandaliwa baada ya mechi hiyo, siku kadhaa kabla ya sherehe 74 ya kuzaliwa kwake. Japo timu yake ilifungwa mabao 5-1 na timu ya Maccabi Ramat Gan, mzaliwa hiyo wa Iraq anasemakana kuwa alionesha mchezo mzuri wakati wa mechi hiyo. "Hii sio fahari yangu pekee bali ni fahari ya Israel michezoni kwa ujumla," Hayik aliliambia shirika la habari la Reuters. Mmoja wa watoto wake wa kiume Moshe Hayi, aliye na umri wa miaka 36, alisifia ufanisi wa baba yake kwa furaha na bashasha"siamini kwa kweli", alisema. Haki mili...

Aanza safari ya kuvuka bahari ya Atlantiki kwa kutumia pipa

Jean-Jacques Savin: Raia wa Ufaransa Jean-Jacques Savin ametumia miezi kadhaa kutengeneza pipa hilo katika chelezo kimoja kusini magharibi mwa Ufaransa Bwana mmoja raia wa Ufaransa ameanza safari ya kuvuka bahari ya pili kwa ukubwa duniani, Atlantiki, kwa kutumia pipa kubwa aliloliunda mwenyewe. Jean-Jacques Savin, mwenye miaka 71, ameanzia safari hiyo kutoka mji wa El Hierro uliopo kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania na anataraji kufika visiwa vya Caribbean ndani ya miezi mitatu. Pipa hilo linategemea nguvu ya msukumo ya mawimbi pekee kufanikisha safari. Ndani ya pipa hilo kuna sehemu ya kulala, jiko na stoo ya kuhifadhi vitu. Bwana Savin pia atakuwa anaweka alama katika safari yake ili kuwawezesha wataalamu wa bahari kuyafanyia tafiti zaid mawimbi ya bahari ya Atlantiki. Taarifa zote kuhusu mwenendo wa safari hiyo zinawekwa kwenye  ukurasa maalumu wa mtandao wa Facebook  na ujumbe wa mwisho umeeleza kuwa pipa lilikuwa linaenda vizuri. Katika mahojiano kwa...