Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HAKI ZA BINADAMU

BONIFACE MWANGI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO 21

Picha
Mwanaharakati mashuhuri anayetetea haki za binaadamu nchini Kenya, Boniface Mwangi atafikishwa Mahakamani kesho Jumatatu Julai 21 kwa madai ya kuchochea vitendo vya Kigaidi. Idara ya Polisi nchini Kenya imethibitisha kumkamata Boniface kwa madai ya kuitisha maandamano yaliyokuwa na vurugu ya kupinga Serikali ya Rais Ruto. Idara ya upelelezi nchini Kenya, DCI imesema katika mtandao wake wa X kwamba maafisa wake wamemkamata Mwangi nyumbani kwake katika kaunti ya Machakos na kupata Mabomu mawili ya kutoa machozi, Mkanda wa risasi, simu mbili za mkononi, Kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu. Boniface Mwangi pia anapaswa kusimamishwa kizimbani kujibu makosa ya kumiliki Silaha kinyume cha sheria. Taarifa za kukamatwa kwake tayari zimezua hasira miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakitaka mwanaharakati huyo kuachiwa huru bila masharti.

Tanzania :- Marekani na Uingereza zatilia shaka 'haki za Binadamu kisheria'

Picha
Tamko la Marekani na Uingereza linagusia kesi ya Erick Kabendera kama mfano wa hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania." Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria. "Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo. "Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria k...

Bunge la Umoja wa Ulaya latoa azimio la kulinda haki za binadamu Tanzania

Picha
Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania. Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja. Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka. Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam. Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia mo...

Mfungwa achagua kuuawa kwa kutumika kiti cha umeme badala ya sindano ya sumu Marekani

Picha
The electric chair has gradually been replaced as the main method of execution Mfungwa mmoja katika jimbo la Tennessee nchini Marekani atauawa kwa kiti cha umeme baada ya kudai kuwa sindano ya sumu itasababisha ateseke. David Earl Miller, ambaye amekuwa kwenye hukumu ya kifo kwa miaka 36 ni kati ya wafungwa wanaoongezeka wanaojaribu kukwepa sindano ya sumu kufuatia visa kadhaa vya kufeli. Mfungwa mwingine huko Tennessee Edmund Zagorski, aliuawa kwa njia ya umeme mwezi uliopita. Kuuliwa kwa kutumia sindano ya sumu ndiyo njia kuu ya kuwaua wafungwa katika jimbo hilo. Hata hivyo wafungwa katika jimbo hilo ambao walitenda uhalifu kabla ya mwaka 1999 wataruhusiwa kuchagua kuuliwa kwa njia ya umeme. Mahakamani, Miller na Zagorski walitaja kisa cha kuuuliwa Billy Ray Irick cha mwezi Agosti ambaye alibadilika rangi kuwa Zambarau na kuchukua dakika 20 kufa. Kuuliwa kwa Zagorski ilikuwa mara ya pili kiti cha umeme kimetumiwa katika jimbo hilo tangu mwaka 1960. Miller alikutwa na ha...