Maeneo nane unayotakiwa kuyatawala kiuhakika ili ufanikiwe Ushindi wowote katika mafanikio unapatikana kwa kutawala. Kwa mfano, Ili uweze kufanikiwa katika biashara unatakiwa kuitawala biashara hiyo katika kila eneo, kwa kuijua biashara hiyo ndani nje tena kwa uhakika. Hata katika mafanikio kwa ujumla vipo vitu ambavyo unatakiwa kuvitawala, kwa jinsi unavyovitawala vitu hivyo unapata uhakika wa mafanikio kwa asilimia kubwa sana. Je, ni mambo yapi ambayo unatakiwa kuyatawala ili kufanikiwa? 1. Jitawale wewe kwanza. Kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukitawala vizuri ili ujijengee mafanikio ni kujua jinsi ya kujitawala wewe. Tambua jinsi ya kutawala fikra zako, matendo yako, vitu unavyosoma au kuangalia, imani na mitazamo uliyonayo juu ya maisha ya mafanikio. Kwa kujua jinsi ya kutawala hayo mambo inakusaidia sana wewe kuweza kufanikiwa na kupiga hatua. Watu wanaofanikiwa wanajua sana jinsi ya kujitawala wao wenyewe hasa kutokana na kumudu kutawala ...