Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya USAFIRI WA ANGA

Moscow yajibu kura ya shirika la Umoja wa Mataifa la usafiri wa anga ya MH17

Picha
Uchunguzi wa kuangushwa kwa ndege hiyo katika anga ya Ukraine mwaka 2014 ulikuwa wa upendeleo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema. Mawakili walihudhuria ukaguzi wa majaji wa ujenzi upya wa mabaki ya MH17 mnamo Mei 26, 2021 huko Reijen, Uholanzi.  ©   Piroschka van de Wouw / Picha za Getty Urusi imekanusha madai ya shirika la Umoja wa Mataifa la usafiri wa anga kwamba ilihusika na kudunguliwa kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysia 2014 mashariki mwa Ukraine. Moscow imesisitiza kuwa uchunguzi unaoongozwa na Uholanzi kuhusu tukio hilo ulichochewa kisiasa na ulitegemea ushahidi  "wa kutiliwa shaka"  uliowasilishwa na Kiev. "Msimamo mkuu wa Moscow unabakia kuwa Urusi haikuhusika katika ajali ya MH17, na kwamba taarifa zote zinazopingana na Australia na Uholanzi ni za uongo,"  Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema kwenye tovuti yake Jumanne. Kauli hiyo ilikuja baada ya Baraza la Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) kupiga kura kwamba Urusi ime...

Miunganisho ya Ndege ya Kimataifa ya Urusi Inapanuka

Picha
Moscow Airport Indonesia itazindua safari za ndege za moja kwa moja hadi Vladivostok katika Mashariki ya Mbali ya Urusi, na njia za usafiri kuelekea miji mingine mikubwa nchini humo, ubalozi wa Indonesia huko Moscow ulitangaza Ijumaa.  "Tutafungua usafiri wa ndege wa moja kwa moja na Jakarta," Berlian Helmi, naibu mkuu wa misheni katika ubalozi wa Indonesia nchini Urusi, aliiambia Tass siku ya Ijumaa, akimaanisha mji mkuu wa Indonesia.  "Kwanza, tutafungua safari ya ndege kati ya Jakarta na Vladivostok, kisha kupitia Vladivostok hadi Moscow, [Jamhuri ya Urusi ya] Bashkortostan, Nizhny Novgorod na Tomsk," alisema.  Makubaliano yote ya lazima na upande wa Urusi tayari yamefikiwa, mwanadiplomasia huyo alisema.  Indonesia iko tayari kuanza safari za ndege hadi Vladivostok punde tu uwanja wa ndege wa eneo hilo utakapothibitisha kuwa uko tayari kuzipokea, aliongeza.  

Mambo yako vipi kwa Air Tanzania hii leo?

Picha
Air Tanzania: Faida ikoje baada ya kufufuliwa shirika la ndege Tanzania? Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai 2018 Wiki hii shirika la ndege nchini- Air Tanzania linaidhinisha njia mpya ya usafiri - jambo linalotazamwa kuwa fursa ya ukuwaji linapokuja sula la usafiri wa abiria. Rais John Pombe Magufuli aliahidi kwamba shirika hilo litaimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani. Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Zambia, Zimbabwe, Nigeria na Uganda, imelifufua shirika lake la ndege, ama kama lijulikanavyo, Air Tanzania. Uwekezaji mkubwa umefanywa mpaka sasa katika kulifanikisha hilo. "Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5. Lakini sasa tumenunua ndege 7, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakuja mwaka 2020", alisema Rais Magufuli mwaka jana 2018 katika  hafla ya ...

URUSI: KUCHUNGUZA ANGA ZA JUU

Picha
Urusi yazindua darubini ya kudhibiti joto la anga Chombo cha Spektr-RG kimetengenezwa kwa muundo wa darubini mbili ndani ya chombo kimoja Moja ya safari muhimu zaidi za kisayansi nchini Urusi kuwahi kushuhudiwa katika baada ya utawala wa utawala wa Kisovieti imezinduliwa kutoka eneo la Baikonur. Spektr-RG telescope chenye darubini ya anga za mbali -ni uvumbuzi uliokamilika kwa ushirikiano na Ujerumani ambayo inatarajia kupima nishati ya joto kote angani na kutoa taarifa. Watafiti wanasema taarifa hii itasaidia kupata muundo wa dunia kwa upana zaidi. Matumaini ni kwamba Spektr-RG kitaweza kutoa mtizamo mpya juu ya upana wa anga. Utengenezaji wa chombo hiki ni safari ya miongo kadhaa kwa wanasayansi wa urusi Kinatarajiwa pia kutambua idadi ya mpya ya vyanzo vya nishati , kama vile mashimo makubwa meusi yaliyopo katikati mwa nyota nyingi. Wakati gesi inapoanguka katika mashimo hayo , huwa na joto kali na kumeguka na kugeuka kuwa joto kali. Mionzi yake hatimae husab...

TCAA yafafanua kuhusu kuzuia ndege za Masha

Picha
Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA nchini imekanusha taarifa ya kuzuiwa kwa ndege za Shirika la Ndege la Fastjet, kama ilivyoelezwa na Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo Laurence Masha, kwa kile ilichokisema ilipokea barua ya shirika hilo Desemba 24 mwaka huu. Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la FastjetLawrence Masha. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema baadhi ya barua za kuomba kuwasilisha ndege hizo zilifikishwa kwao Desemba 24 na hazikushughulikiwa kutokana na kuwa ni kipindi cha sikukuu. " Nakanusha taarifa si za kweli hatujawahi kukataa ombi la kuleta ndege na hatuwezi kukataa kwa sababu ni maagizo tuliyowaambia ." amesema Johari. " Walileta andiko la mabadiliko ya utawala na fedha tarehe 24 Desemba mwaka huu , na wataalamu wameanza kulifanyia kazi na muda si mrefu tutawajibu ," ameongeza. Aidha Mkurugenzi huyo amesema miongoni mwa masharti am...

Boeing 787-8 Dreamliner: Mambo matano makuu aliyoyasema Magufuli kuhusu ndege mpya ya Tanzania

Picha
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Jumapili aliongoza taifa hilo kupokea ndege mpya ya kisasa ambayo imenunuliwa kwa ajili ya kutumiwa na shirika la ndege la taifa hilo. Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL). Bei ya ndege hiyo inakadiriwa kuwa $224.6 milioni (Sh512 bilioni za Tanzania) kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti ya kampuni ya Boeing. Ndege hiyo iliwasili majira ya saa 11:10 jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kisha kupewa heshima ya kumwagiwa maji na baadaye Rais Magufuli akiwa na viongozi wakuu walioambatana naye akaizindua rasmi. Aidha, yeye na Makamu wake Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, waliikagua kwa kuingia ndani ya ndege ili kujionea mandhari ya ndani. Mataifa ya Afrika yaliyo na Dreamliner Ethiopia (Ethiopian Airlines )*- 19 Kenya (Kenya Airways) - 8 Morocco ...