MTEULE THE BEST Nani alihusika katika shambulio la kirusi cha mtandaoni ambacho kiliathiri kompyuta katika zaidi ya mataifa 150 duniani, zikiwemo Kenya na Tanzania? Kumeibuka madai kwamba huenda wadukuzi walitoka Korea Kaskazini. Lakini kufikia sasa, hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha hilo. Huenda hujawahi kusikia kuhusu kundi linaloitwa Lazarus Group, lakini pengine unafahamu baadhi ya matokeo ya shughuli zake. Kundi hili lilihusika katika kudukua mfumo wa kompyuta wa Sony Pictures mwaka 2014 na tena wakadukua benki moja ya Bangladesh mwaka 2016. Inasadikika kwamba wadukuzi hao wa Lazarus Group walifanyia kazi yao China lakini kwa niaba ya Korea Kaskazini. Wataalamu wa usalama mtandaoni sasa wanahusisha shambulio la kirusi cha WannaCry na kundi hilo baada ya ugunduzi uliofanywa na mtaalamu wa usalama wa kompyuta wa Google Neel Mehta. Mehta aligundua kwamba maelezo ya kutunga programu ya kompyuta ya kirusi cha WannaCry yanafanana na maelezo ya programu zilizowahi...