Urusi inakana kuunda silaha zinazokiuka mkataba huo Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka mkataba mpya wa nyuklia usainiwe na Russia na China kwa pamoja. Bwana Trump amesema amekuwa akizungumza na na nchi hizo mbili kuhusu wazo hilo na wote "walilifurahia sana sana". Kauli zake Trump zinakuja baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba muhimu wa nyuklia na urusi , ikielezea juu ya aina mpya ya silaha. Enzi ya Vita Baridi mkataba wa zana za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987. Mkataba huo (INF) ulipiga matrufuku matumizi ya zana za masafa ya kati yanayopiga kilomita 500 hadi 5,500 (310-3,400 miles). Kujiondoa kwa Marekani kwenye mkataba huo Ijumaa kumefuatia shutuma za marekani kwamba Urusi ilikuwa imekiuka mkaataba huo kwa kuunda mtambo mpya wa mfumo makombora . Moscow imekanusha haya. Akijibu maswali juu ya ni vipi ataepuka silaha za nyuklia kufuatia kuvunjika...