Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 20, 2018

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika, Mazungumzo hayo yalifanyika upande wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom. Bw Moon atatangaza matokeo ya mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi. Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea na kumaliza misukosuko

UEFA Ligi ya Mabingwa Ulaya Champions League: Nani atawika fainali Kiev kati ya Salah, Ronaldo na Milner?

Mohamed Salah, Cristiano Ronaldo na James Milner Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi itakuwa kati ya timu ambazo zimefunga mabao mengi zaidi msimu huu huku washambuliaji bora zaidi duniani wakikutana. Real Madrid wanatafuta ushindi wa 13 na wa tatu mfulizo huku Liverpool wakiweza kupanda juu ya Bayern Munich na Barcelona nyuma na AC Milan katika orodha ya vilabu vilivyopata ushindi mara nyingi zaidi katika European Cup na Champions League ikiwa wataibuka washindi huko Kiev. Milner anaweza kuwa na umuhimu usiotarajiwa Kiev? Zikiwa zimefunga zaidi ya mabao 90 kwenye mashindano yote msimu huu ni wazi kuwa fainali hii itakuwa kama vita kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool. Wote wako mbioni kun'gang'ania tuzo ya Ballon d'Or mwishoni mwaka 2018, lakini pia kuna mwanamume ambaye bila kutarajiwa huenda akawa mwenye umuhimu mkubwa huko Kiev. James Milner alionyesha ubabe wakati wa nusu fainali dhidi ya Roma wakati a...

Iran yatoa masharti kuhusu mwafaka wa nyuklia

Iran inataka mataifa ya Ulaya kuwafidia ifikapo mwisho wa mezi Mei baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015, kwa mujibu wa afisa mwandamizi. Iran itaamua iwapo itasalia kwenye mpango huo. Makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni yaliondoa vikwazo dhidi ya Iran huku taifa hilo likitakiwa kusitisha mpango wake wa nyuklia. Tangu Rais Donald Trump aiondoe Marekeni kwenye makubaliano hayo mwezi uliopita, mataifa ya Ulaya yamekuwa yakijaribu kuhakikisha kuwa Iran inafaidika kiuchumi ili kuishawishi kuendelea kusalia kwenye mwafaka huo. Lakini jambo hilo linasalia kuwa changamoto baada ya kampuni za Ulaya kutishwa na vikwazo vya Marekani. Mataifa yaliyosalia kwenye mwafaka huo yanakutana Ijumaa (25.05.2018) kwa mara ya kwanza tangu Trump kujindoa kwenye makubaliano hayo, lakini wanadiplomasia hawaoni mwafaka huo ukidumishwa. Maofisa wa Uingereza, Uchina, Ufaransa, Ujerumani na Urusi wanakutana na naibu waziri wa masuala...

WHO yatoa tahadhari kuhusu watu kuumwa na nyoka

Mashambulizi ya nyoka yameleta madhara makubwa duniani Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani. Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO , kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka. Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote. Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha. Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa...

Trump asema Korea Kaskazini imetoa majibu ya "ukarimu", "ufanisi"

Rais Donald Trump Rais Donald Trump amesema Ijumaa asubuhi kuwa Korea Kaskazini imetoa mrejesho wa “ukarimu” na “ufanisi" baada ya kusitisha mkutano wake na Kim Jong Un. “Ni habari nzuri sana kupokea kauli ya mrejesho ya upole na ufanisi kutoka Korea Kaskazini,” Trump amesema katika ujumbe wa Twitter Ijumaa asubuhi. “Hivi karibuni tutafahamu kile kitakachoendelea, ni matumaini yangu itakuwa ni utajiri na amani ya kudumu na ya muda mrefu. Ni wakati peke yake (na kipaji) utatuthibitishia hili. Korea Kaskazini imesema Ijumaa bado iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani” wakati wowote, [katika] mpangilio wowote.” Makamu Waziri wa Mambo ya Nje Kim Kye Gwan, mwakilishi katika mazungumzo ya nyuklia wa muda mrefu na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, amesema katika tamko lililotangazwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini iko “tayari kuipa Marekani muda na fursa” kufikiria suala la mazungumzo. Trump alijitoa ...

Uholanzi, Australia zaituhumu Urusi kuidungua ndege ya MH17

Uholanzi imeiambia Urusi kwamba itaishitaki kwa jukumu lake katika kuangushwa kwa ndege ya Malaysia yenye nambari za safari MH17 tarehe 17 Julai 2014 baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa kombora la Urusi ndio lililotumika. MH17 ilidunguliwa ikiwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine wakati ikiwa angani kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur, na kuuwa watu wote 298 waliokuwemo, ambapo karibu theluthi mbili walikuwa raia wa Uholanzi. Timu ya wachunguzi wa kimataifa ilisema siku ya Alhamisi kuwa mfumo wa makombora wa "Buk" uliotumiwa kuidungua ndege hiyo ya abiria ulitoka kwenye brigade ya 53 ya mashambulizi ya ndege, yenye makao yake katika mji wa Magharibi mwa Urusi wa Kursk. "Hii ndiyo mara ya kwanza taifa makhsusi kunyooshewa kidole," waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri. "Tunaitwika lawama Urusi kwa ushiriki wao katika kupe...

Korea Kaskazini yasema iko tayari kuzungumza na Marekani

Korea Kaskazini yasema bado ipo tayari kuzungumza na Marekani hata baada ya rais Donald Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na Kim Jong Un. Rais Trump alieleza hapo jana kwamba hatakutana na Kim Jong Un na sababu aliyoitoa ni kuwepo mazingira ya ghadhabu na uhasama wa wazi. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Kim Kye Gwan amesema nchi yake imesikitishwa na uamuzi huo wa Marekani. Mkutano huo ulionekana kama fursa ya kihistoria kwa Marekani kuweza kuishawishi Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa silaha za nyuklia na siku ya Alhamisi, waandishi wa habari wa kimataifa walishuhudia Korea Kaskazini ilipokifunga kituo chake kikuu cha kufanyia majaribio ya nyuklia. Wakati Korea Kaskazini ilipotoa kauli kali dhidi ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton, kauli hiyo ndio ilikuwa sababu ya Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kiongoz...

Kombora lililoidungua ndege ya Malaysia lilikuwa la Urusi

Sehemu ya mabaki ya ndege Kombora lililodungua ndege ya shirika la ndege la Malaysia mashariki mwa Ukrain mwaka 2014 lilikuwa na Urusi, wachunguzi wa kimataiafa wamesema. Kwa mara ya kwanza timu ya wachunguzi ikiongozwa na Uholanzi imesema kombora hilo lilitoka kwa kikosi cha Urusi kilicho mji wa Kursk. Watu wote 298 waliokuwa ndani ya ndege ya Boeng 777 waliuawa wakati ilivunjika vipande ikiwa safarini kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur. Ilipigwa na kombora aina ya BUK lililofyatuliwa kutoka eneo lililodhitiwa na waasi nchini Ukrain. Urusi inasema hakuna silaha zake zilizotumika. Sehemu ya mabaki ya ndege Lakini leo Alhamisi Wilbert Paulissen, afisa wa Uholanzi kutoka kundi la wachunguzi la pamoja JIT, aliwaambia waandishi wa habari kuwa magari kwenye msafara uliobeba kombora hilo ulikuwa sehemu ya jeshi la Urusi. Alisema wachunguzi walikuwa wamefuatilia msafara huo na kugundua kuwa ulikuwa wa kikosi wa 53 cha jeshi la Urusi ' Kisa hicho kilito...

Ushawishi wa China na Urusi Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mataifa ya Urusi na china yanaingia kwa nguvu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku ushawishi wa Ulaya katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa madini na kieneo ukiendelea kupungua kwa mujibu wa wachambuzi. Umoja wa Mataifa umeliweka taifa hilo katika nafasi ya miwsho kwenye nchi 188 zilizotajwa katika faharasi ya maendeleo ya kibinadamu huku mizozo ikishuhudiwa. Sehemu kubwa ya taifa hilo liko kwenye himaya ya waasi. Sehemu kubwa ya nchi hiyo iko mikononi mwa makundi ya wanamgambo na vurugu zimesababisha robo ya wakaazi wake  milioni 4.5  kuyakimbia makaazi yao. Pamoja na kuonekana kuwa taifa masikini kuna utajiri mkubwa uliotapakaa kuanzia madini ya almasi na dhabu hadi shaba na Urani ambayo yanapatikana katika maeneo mengi ya nchi hiyo. Ufaransa koloni la zamani la nchi hiyo ndiyo nchi tangu jadi ikiyaingia masuala ya Jamhuri ya Afrika ya kati. Iliingia kijeshi mwaka 2013 baada ya kiongozi wa muda mrefu Francois Bozize kuondolewa kwa nguvu madarakani na kundi la ...

Merkel na Li watetea makubaliano na Iran

Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel na waziri mkuu  wa China Li Keqiang wametetea makubaliano ya kinyuklia na Iran, wakati Li  akisema kusitisha makubaliano hayo kutaleta utata katika majadiliano na Korea kaskazini. Merkel   na  Li  walionesha  msimamo  wa  pamoja  kuelekea  Iran pamoja  na  biashara  huru, masuala  mawili  ambayo  yameshuhudia uingiliaji  kati  wa  Marekani  ambapo  rais  Donald Trump  alichukua hatua  hiyo. Hayo  yalijadiliwa  katika  mkutano  wao  katika  ziara ya  kansela  Merkel  mjini  Beijing. waziri mkuu wa China Li Keqiang (kushoto) akizungumza na kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kulia) Li  alionya  kwamba  kusitisha makubaliano  hayo  na  ...

Unai Emery: Ninataka Arsenal wawe klabu bora zaidi duniani

Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery amesema anataka klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu bora zaidi Ulaya kwa mara nyingine, na hata bora duniani. Alisema hayo alipohutubiwa wanahabari kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa mrithi wa Arsene Wenger. Mkufunzi huyo wa miaka 46 aliwasilishwa rasmi kwa mashabiki na wanahabari Jumatano kabla yake, akiandamana na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis kuhutubia waandishi wa habari waliokuwa wamefika kwa wingi. Alisema: "Ufanisi msimu ujao utakuwa bado tunaukuza, lakini kwa jinsi gani? Kwa kupigania kila taji. "Hilo limo ndani ya historia ya Arsenal na yangu mwenyewe." Arsenal walishindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2017 na hawatashiriki michuano hiyo msimu wa 2018-2019. Awali, walikuwa wamefuzu kila mwaka tangu 1998. Mhispania huyo Gazidis alifichua kwamba Mhispania huyo alikuwa kwenye orodha ya wakufunzi wanane ambao walikuwa wamewekwa kwenye mizani kumtafuta mtu wa kumrithi Wenger, lakini ye...

Itai Dzamara: Mwanamume aliyempinga Robert Mugabe na akatoweka

Dzamara Itai Dzamara mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Robert Mugabe kabla hajatoweka. Miaka mitatu baadaye wapendwa wake bado wanasubiri majibu. Sheffra Dzamara hajamuona mume wake kwa zaidi ya miaka mitatu. Maisha yake yalibadilika ghafla tarehe 9 Machi mwaka 2015 wakati Bw Dzamara alitekwa nyara. Tangu wakati huo ameishi maisha yaliyojaa giza pasipo kujua ikiwa yuko hai au amekufa. 'Huwa ninatabasamu' Licha ya kutokuwepo kwake Bw Dzamara bado yuko chumbani walimokuwa wakiishi kwenye mtaa unaojulikana kama Glen Norah huko Harare. Sehemu moja ya nyumba yao kuna picha yake. Kwenye picha hizo Bw Dzamara na mke wake wanaonekama wakitabasamu, ishara ya vile siku zao zilikuwa nzuri,. Maisha tangu mumuwe atoweka hajakuwa rahisi. "Kwa kusema ukweli ninahisi mpweke," Bi Dzamara anasema. Hata hivyo ni lazima aonyeshe sura ya ujasiri kwa mtoto wao wa kiume wa miaka 10 na msichana wa umri wa miaka mitano. "Wakati sina raha wanafah...

Korea Kaskazini yamuita 'mjinga' Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence

Korea Kaskazini yamuita Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence 'mjinga' Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa "mjinga" na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli. Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo. Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa. Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo. Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita. Silaha za nyuklia zimekuwa ajenda kuu kwa miaka mingi kwa Korea Kaskazini Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea...

Man Utd ndiyo klabu yenye thamani kubwa zaidi Ulaya

Manchester United na Chelsea zote zimo kwenye 10 bora Manchester United kwa mara nyingine wametangazwa kuwa klabu yenye thamani ya juu zaidi Ulaya, ambapo thamani yao inakadiriwa kuwa €3.25bn (£2.9bn) kwa mujibu wa kampuni ya KPMG. Klabu hiyo ya England inaongoza kwa "thamani ya biashara", ikiwa mbele ya klabu nyingine kama vile Real Madrid na Barcelona. Orodha hiyo imeandaliwa baada ya utafiti uliofanywa kwa kuangazia taarifa za kifedha za misimu ya 2015-16 na 2016-17 ambapo waliangazia faida, haki za utangazaji, umaarufu, matarajio kutokana na uwezo wa kimichezo na thamani ya uwanja. Liverpool, ambao wamefika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wamo nafasi ya nane kwenye orodha hiyo. Kwenye utafiti huo ulioangazia klabu 32 kubwa, klabu za Ligi Kuu ya England zinajaza nafasi sita kati ya 10 za kwanza. Andrea Sartori, mkuu wa michezo duniani katika KPMG ambaye ndiye mwandishi wa ripoti hiyo, anasema kwa jumla thamani ya klabu za soka imepanda katika mwaka ...

Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa naibu katibu mkuu wa UNEP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira duniani, UNEP. Afisi kuu za shirika hilo la UN huwa jijini Nairobi, Kenya. Bi Msuya atachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu. Hadi wakati wa kuteuliwa kwake Jumatatu, Bi Msuya alikuwa mshauri wa Makamu Rais wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Asia Mashariki na Pacific jijini Washington, DC wadhifa alioushikilia tangu mwaka jana. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, kwa mujibu wa UN alisema "Bi Msuya analeta uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye nyanja za maendeleo ya kimataifa kuanzia masuala ya mashirika, mikakati, uendeshaji, ufahamu wa usimamizi na ubia alioupata wakati akifanya kazi huko Afrika, Amerika Kusini na Asia." Alishika nyadhifa mbalimbali katika ngazi ya uandamizi kwenye Benki ya Dunia ikiwemo mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mkuu wa...

Maduro ashinda uchaguzi Venezuela

Tume ya uchaguzi wa Venezuela imemtangaza Rais Nicolas Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Jumapili, ambao ulisusiwa na upinzani. Kulingana na tume hiyo, Maduro amepata zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa. Ni matokeo ambayo hayakuwashangaza watu kwa sababu chama kikuu cha upinzani kiliususia uchaguzi huo, na kisha, wapinzani wawili wakuu wakazuiwa kugombea. Na siyo hayo tu, kwa sababu hata tume ya uchaguzi inaripotiwa kuendeshwa na washirika wa karibu wa Rais Nicolas Maduro. Tume hiyo imesema Maduro aliungwa mkono kwa kura milioni 5.8 ambazo ni sawa na asilimia 67.7, akifuatiwa kwa mbali na Henri Falcon, gavana wa zamani wa jimbo ambaye alikihama chama tawala cha kisoshalisti mwaka 2010, aliyepata kura milioni 1.8, sawa na asilimia 21.2. Katika nafasi ya tatu yuko mhubiri wa kievanjelisti Javier Bertucci, aliyeambulia asilimia 11 ya kura zilizopigwa. Akiuhutubia umati wa wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Rais Maduro alisema wapinzani wake walijidangan...