UEFA Ligi ya Mabingwa Ulaya Champions League: Nani atawika fainali Kiev kati ya Salah, Ronaldo na Milner?
Mohamed Salah, Cristiano Ronaldo na James Milner
Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi itakuwa kati ya timu ambazo zimefunga mabao mengi zaidi msimu huu huku washambuliaji bora zaidi duniani wakikutana.
Real Madrid wanatafuta ushindi wa 13 na wa tatu mfulizo huku Liverpool wakiweza kupanda juu ya Bayern Munich na Barcelona nyuma na AC Milan katika orodha ya vilabu vilivyopata ushindi mara nyingi zaidi katika European Cup na Champions League ikiwa wataibuka washindi huko Kiev.
Milner anaweza kuwa na umuhimu usiotarajiwa Kiev?
Zikiwa zimefunga zaidi ya mabao 90 kwenye mashindano yote msimu huu ni wazi kuwa fainali hii itakuwa kama vita kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool.
Wote wako mbioni kun'gang'ania tuzo ya Ballon d'Or mwishoni mwaka 2018, lakini pia kuna mwanamume ambaye bila kutarajiwa huenda akawa mwenye umuhimu mkubwa huko Kiev.
James Milner alionyesha ubabe wakati wa nusu fainali dhidi ya Roma wakati alifikisha mchango wake muhimu katika mechi hadi mara 8 msimu huu na kusawazisha rekodi iliyowekwa na Neymar mwaka 2016-17.
Ni nani anakumbwa na harakati zaidi katika safu ya ulinzi?
Wakati wa kuanza kwa msimu kulikuwa na shaka kuhusu safu ya ulinzi ya Liverpool, lakini kufuatia kuwasili kwa Virgil van Dijk mwezi Januari na kuimarika kwa kipa Loris Karius inamaanisha kuwa tena hakuna udhaifu.
Kwa Real ni kitu tofauti.
Walikosa mchango wake Sergio Ramos wakati wa duru ya pili ya mechi kati yao na Juventus.
Liverpool nao wana matatizo yao, wameshindwa mara 13 kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ikiwemo mara sita dhidi ya Roma na sare yao ya mwisho.
Lakini kikosi hicho cha Jurgen Klopp kimeshinda mara sita mfululizo msimu huu rekodi iliyowekwa na Barcelona.
Maoni