Dzamara
Itai Dzamara mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Robert Mugabe kabla hajatoweka. Miaka mitatu baadaye wapendwa wake bado wanasubiri majibu.
Sheffra Dzamara hajamuona mume wake kwa zaidi ya miaka mitatu. Maisha yake yalibadilika ghafla tarehe 9 Machi mwaka 2015 wakati Bw Dzamara alitekwa nyara.
Tangu wakati huo ameishi maisha yaliyojaa giza pasipo kujua ikiwa yuko hai au amekufa.
'Huwa ninatabasamu'
Licha ya kutokuwepo kwake Bw Dzamara bado yuko chumbani walimokuwa wakiishi kwenye mtaa unaojulikana kama Glen Norah huko Harare.
Sehemu moja ya nyumba yao kuna picha yake.
Kwenye picha hizo Bw Dzamara na mke wake wanaonekama wakitabasamu, ishara ya vile siku zao zilikuwa nzuri,.
Maisha tangu mumuwe atoweka hajakuwa rahisi.
"Kwa kusema ukweli ninahisi mpweke," Bi Dzamara anasema.
Hata hivyo ni lazima aonyeshe sura ya ujasiri kwa mtoto wao wa kiume wa miaka 10 na msichana wa umri wa miaka mitano.
"Wakati sina raha wanafahamu kwa hivyo ni lazima nijaribu kutabasamu na kuwa na furaha."
Dzamara aliondolewa kutoka kinyozi kimoja kilicho karibu na nyumbani kwake mwezi Machi mwaka 2015
"Ni hali ngumu sana kwao kwa sababu mara kwa mara wao huniuliza kuhusu baba yao. Hata leo mvulana amenishangaza kwa kuvaa kofya ya baba yake kwa mara ya kwanza. Unaweza kuona wazi kwa kweli amemkosa," Bi Dzamara anasema.
Mwaka 2014 Bw Dzamara alianzisha vuguvugu katika hatua ambayo ilikuwa hatarai sana. Wapinzani wa kisiasa mara nyingi hulipia vitendo vyao.
Lakini siku baada ya siku Bw Dzamara alirudi kupiga kambi kwenye bustani Africa Unity Square, bustani ambayo imejaa miti kati kati mwa mji wa Harare, akiwa na bango lililosema "Mugabe amefeli ni ni lazima aondoke madarakani."
Baadaye watu wengine wakajiunga naye.
Dirk Frey ambaye mara ya kwanza alifahamu hilo kupitia mitanao anakumbuka jinsi walikimbizana na polisi wakati wa maandamana yao ya mchana.
Bw Dzamara anasema alipigwa hadi kuzirai na kundi la polisi 20 miezi kabla, Novemba 2014
Vitendo hivyo vidogo vilikuja na malipo mabaya. Bw Dzamara alilazwa hospitalini mara kadhaa baada ya kupigwa na polisi.
Kisha Oktoba 17 mwaka 2014 alipeleka maandamano yake mbali. Yeye na wenzake wawili Tichaona Danho na Philosophy Nyapfumbi walikuwa wamepeleka azimio kwa ofisi ya Mugabe wakimtaka aondoke madarakani.
Walihojiwa kwa saa nane na kupigwa. Kisa hicho kilipata umaarufu kwenye umma na hata kuandikwa na magazeti. Chini ya miezi sita alitoweka.
Kutoweka
Mtu wa mwisho aliyemuona Dzamana ambaye ni kinyozi wake bado anakumbuka kile kilichotokea.
Asubuhi hiyo alikuwa kwenye kinyozi chake kilicha umbali wa dakika chache kutoka nyumbani kwake Dzamara.
Bw Dzamara alikuwa kwenye kinyozi hicho akinyolewa ndevu wakati waliona gari nyeupe ambayo ilionekana kuzunguka jengo kilipokuwa kinyozi.
Ilionekana ikitafuta kitu fulani lakini Bw Dzamara aliokena kufamua walikuwa ni nani.
Marafiki na familia wamekuwa wakifanya maandamano kadhaa kutaka kujua kilichomfanyikia Itai Dzamara
"Ndeye vakonama" alisema, ambayo ni lugha ya Shona ikimaanisha "gari hilo ni la vijana".
"Vijana" walikuwa na kikosi cha siri cha polisi wa Zimbabwe.
Dakika chache baadaye wanaume wawili waliokuwa wamevaa kiraia wakaingia na kuuliza wauziwe salio la simu zao.
Wakati kinyozi alisema hakuwa nayo, wanaume hao wakasema kuwa walikuwa wanamtafuta mwizi wa ng'ombe- Bw Dzamara.
Gari hilo likaondoka kwa kasi na jumla ya wanaume watano walihusika na utekaji nyara huo wa Bw Dzamara tangu wakati huo hajaonekana
Maoni