Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 29, 2017

WATAMBUE WACHEZAJI 30WALIO CHAGULIWA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRICA

Walioteuliwa katika orodha hiyo ni: 1. Ali Maaloul (Tunisia na Al Ahly) 2. Bertrand Traore (Burkina Faso na Lyon) 3. Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal) 4. Christian Atsu (Ghana na Newcastle) 5. Christian Bassogog (Cameroon na Henan Jianye) 6. Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns) 7. Eric Bailly (Cote d'Ivoire na Manchester United) 8. Essam El Hadary (Egypt na Al Taawoun) 9. Fabrice Ondoa (Cameroon na Sevilla) 10. Fackson Kapumbu (Zambia na Zesco) 11. Jean Michel Seri (Cote d'Ivoire na Nice) 12. Junior Kabananga (DR Congo na Astana) 13. Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord) 14. Keita Balde (Senegal na Monaco) 15. Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor) 16. Mbwana Samata (Tanzania na Genk) 17. Michael Olunga (Kenya na Girona) 18. Mohamed Salah (Egypt na Liverpool) 19. Moussa Marega (Mali na Porto) 20. Naby Keita (Guinea na RB Leipzig) 21. Percy Tau (South Africa na Mamelodi Sundowns) 22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Borussia Dortmund) ...

CIA yatoa faili 470,000 za Osama Bin Laden

Shirika la ujasusi la Marekani CIA limetoa karibu faili 470,000 zilizopatikana wakati wa kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden mwaka 2011. Faili hizo mpya ni pamoja na stakabadhi kuhusu mipango yake binafsi na video ya mtoto wake wa kiume Hamza wakati wa hasuri yake. Marekani kumsaka mtoto wa Osama Makamando wa Marekani wavamia al-Qaeda Yemen Hii ndiyo mara ya nne CIA inatoa faili za Osama zilizopatikana wakati wa uvamizi kwenye maficho yake huko Abbottabad nchini Pakistan. Hata hivyo faili zingine haziwezi kutolewa kwa sababu zinaweza kuathiri usalama wa tiafa. Kulingana na CIA faili hizo zinafichua uhusiano uliopo sasa kati ya al-Qaeda na ISIS na migawanyiko kati ya al-Qaeda na washirika wake. Kampiuta iliyopataiaka wakati wa uvamizi huo ilikuwa na filamu za Hollywood, vipindi vya watoto na makala tatu kumhusu Osama Bin Laden. Mwana wa Osama bin Laden asakwa na Marekani Video nyingine ni ya harusi na mtoto wa Osama, Hamza Bin Laden akiwa mdogo. Hamza Bin...

Aliyetekeleza shambulizi la New York afikishwa mahakamani

Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamiaji kutoka nchini Uzbek anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani. Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kuwasambazia vifaa kundi la kigaidi la Islamic State. Waendesha mashtaka mjini New York wamefungua mashtaka dhidi ya mhamaji kutoka nchini Uzbestan anayedaiwa kuhusika katika shambulio la gari dogo la mizigo lilitokea jana na kuua watu nane katika mji wa New York nchini Marekani. Sayfullo Saipov anakabiliwa na mashtaka ya kusaidia kutoa vifaa kwa kundi la kigaidi la Islamic State. Akizungumzia mashataka yaliyofunguliwa kaimu mwanasheria mkuu JOON Kim amesema Saipov amefunguliwa mashitaka ya makosa mawili ya ugaidi. Shitaka la kwanza ni kutoa vifa vya kusaidia maandalizi ya shambulio la kigaidi kwa kundi la IS, na shitaka la pili kusababisha uharibifu wa magari...

SIO HABARI: SHILOLE

MTEULE THE BEST

Unbelievable Saves by David De Gea

MTEULE THE BEST

Makundi ya upinzani Syria yapinga mkutano wa amani uliofadhiliwa na Urusi

Licha ya Urusi kujitoa kudhamini mkutano wa amani ili kufikia makubaliano ya kisiasa kuhusu mgogoro wa Syria, wapinzani nchini humo wameukataa mkutano huo wakisisitiza ufanyike Geneva, chini ya Umoja wa Mataifa. Rais wa Urusi, Vladmir Putin Wakati huo huo, Waturuki wameuwekea mgomo mualiko wa Wasyria walio upande wa Wakurdi, huku juhudi hizo za kuleta amani zikikabiliwa na vikwazo siku ya Ijumaa. Licha ya kushiriki kimaamuzi katika vita vya Syria mwaka 2015 ikiwa upande wa Rais Bashar Al-Assad, Urusi sasa inaamini itajiimarisha kutokana na anguko la Dola la kiislamu IS, kwa kuzindua mchakato mpya wa kisiasa utakaopelekea kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miaka sita. Damascus imesema ipo tayari kuhudhuria mkutano wa Sochi utakaofanyika Novemba 18 ambao umepanga kuangazia katiba mpya na kusema kuwa ni wakati sahihi, shukrani kwa ushindi wa jeshi la Syria na kusambaratishwa kwa ugaidi. Lakini maafisa wa upande unaompinga Rais Assad, wameukataa mkutano huo na kusisitiza kuwa mazungu...

Viwango vya ajali vyashuka kwa asilimia 48 Tanzania

Viwango vya ajali vyashuka kwa asilimia 48 Tanzania Ajali za barabarani zimepungua kwa asilimia 48 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2017 ikilinganishwa na kipindi kama hicho 2016 kwa mujibu wa mkuu wa idara ya trafiki nchini Tanzania Fortunatus Musilimu. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi, ajali za barabarani zilishuka kwa 1,264 ambayo ni asilimia 48. Hii ni kutoka 2,639 zilizorekodiwa 2016 hadi 1,375 mwaka huu. Kulingana na afisa huyo vifo na majeraha yalishuka kwa 239 ambayo ni asilimia 32 na 974 ambayo ni asilimi 40 mtawalia. Akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani, alisema kuwa kushuka kwa viwango hivyo kunatokana na juhudi za idara ya polisi wa trafiki, iliotilia mkazo sheria za trafiki mbali na kuhamasisha madereva na uma kuhusu sheria hizo. ''Tumekuwa tukitoa hamasa kupitia mipango kadhaa ikiwemo ule wa wiki ya usalama barabarani.Pia ninawaahidi kwamba nitaw...

Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya

MTEULE THE BEST Raia 2 wa Tanzania na 10 wa Iran wakamatwa kwa dawa za kulevya Raia 10 wa Iran na wawili wa Tanzania wameshtakiwa kwa kuingiza kinyume na sheria takriban kilo 100 za dawa za kulevya aina ya heroine kupitia bahari hindi kulingana na gazeti la The Citizen nchini tanzania. Kulingana na gazeti hilo 12 hao walikamatwa wakiabiri boti kwa jina dhow lililobeba dawa hiyo katika pwani ya Zanzibar Jumanne iliopita wakati maafisa wa shirika la kukabiliana na mihadarati wakishirikiana na maafisa wa usalama walipokuwa wakipiga doria za vita dhidi ya dawa za kulevya. Mahakama ya eneo la Kisutu iliambiwa kwamba washukiwa hao walikamatwa katika maji ya Tanzania mnamo tarehe 25 mwezi Novemba walipokuwa wakipenyeza kilo 111.2 za dawa ya heroine , iliochanganywa na bangi . Hakimu wa mahakama hiyo alikataa ombi la washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana. Wakati wa kukamatwa kwao katika maji makuu , washukiwa hao walidaiwa kutaka kubadili mwelekeo baada ya kubaini kwamba wamenaswa lak...

Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York

MTEULE THE BEST Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo. Bill amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo. Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyewtekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi. Jimmy Carter: Nitaenda Korea Kaskazini kwa niaba ya Trump Je nchi iliyozungumziwa na Trump ya "Nambia" iko wapi? Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule. Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii. Polisi mjini humo wametoa ta...

Cuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani

MTEULE THE BEST Cuba yakana kuwashambulia kwa sauti wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani Cuba inasema kuwa hakujakuwa na mashambulizi ya kutumia sauti dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani kwenye mji wake mkuu Havana, ikisema kuwa madai hayo ni kisiasa yenye lengo la kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Cuba Bruno Rodriguez alipinga madai hayo ya kuwepo mashambulizi ya sauti akiyataja kuwa kuwa uwongo. Marekani yatathmini kufunga ubalozi wake Cuba Marekani inasema kuwa karibu wafanyakazi wake 20 katika ubalozi wake walikumbwa na matatizo ya kiafya na kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na kisa hicho. Ripot zinasena kwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na mashambulizi ya sauti lakini hata hivo hakuna kile kimethibitishwa. Marekani haijailaumu Cuba kwa mashambulizi hayo, na serikali ya Cuba imekana mara kwa mara kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi. wa Marekania mjini Cuba. Marekani iliwatimua wanadiplomasia watano wa Cuba, ikis...