Licha ya Urusi kujitoa kudhamini mkutano wa amani ili kufikia makubaliano ya kisiasa kuhusu mgogoro wa Syria, wapinzani nchini humo wameukataa mkutano huo wakisisitiza ufanyike Geneva, chini ya Umoja wa Mataifa.
Rais wa Urusi, Vladmir Putin
Wakati huo huo, Waturuki wameuwekea mgomo mualiko wa Wasyria walio upande wa Wakurdi, huku juhudi hizo za kuleta amani zikikabiliwa na vikwazo siku ya Ijumaa.
Licha ya kushiriki kimaamuzi katika vita vya Syria mwaka 2015 ikiwa upande wa Rais Bashar Al-Assad, Urusi sasa inaamini itajiimarisha kutokana na anguko la Dola la kiislamu IS, kwa kuzindua mchakato mpya wa kisiasa utakaopelekea kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miaka sita.
Damascus imesema ipo tayari kuhudhuria mkutano wa Sochi utakaofanyika Novemba 18 ambao umepanga kuangazia katiba mpya na kusema kuwa ni wakati sahihi, shukrani kwa ushindi wa jeshi la Syria na kusambaratishwa kwa ugaidi.
Lakini maafisa wa upande unaompinga Rais Assad, wameukataa mkutano huo na kusisitiza kuwa mazungumzo yoyote ya amani yanatakiwa yawe chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa, Geneva, ambako mazungumzo mengine ya amani yamefeli kuleta mafanikio ya kumaliza mgogoro huo tangu ulipozuka mwaka 2011.
Wanajeshi wa ulinzi wa Israel wakiwa katika mpaka wa Syria
Mkutano huo unatajwa kuwa ni mkutano ``Kati ya serikali na serikali`` amesema Mohammad Alloush, mwanachama wa Kamati ya Juu ya majadiliano ya upinzani na Ofisa Mkuu wa kundi la waasi wa la Jaish al- Islam.
Aloush aliiambia Reuters kuwa kamati hiyo ilishangazwa kuona imewekwa katika orodha ya makundi yaliyoalikwa katika mkutano huo na wakasema watatoa tamko pamoja na vyama vingine kueleza kuwa wanakataa mkutano huo.
Makundi yasema mkutano huo ni kukwepa mabadiliko ya kisiasa
Muungano wa makundi ya upinzani ya nchini Syria, wenye makao yake nchini Uturuki, (SNC) umesema mkutano huo ni jaribio la kukwepa ``shinikizo la kimataifa la mabadiliko ya kisiasa`` nchini Syria.
``Muungano hautashiriki katika majadiliano yoyote na serikali nje ya Geneva au bila udhamini wa UN`` msemaji wa SNC; Ahmad Ramadan, ameliambia Reuters.
Mjumbe wa majadiliano wa Urusi, amesema kuwa makundi ya Syria yalioamua kukataa mkutano huo yanajiweka katika hatari ya kuachwa wakati mchakato huo wa kisiasa ukiendelea mbele.
Urusi imealika makundi 33 ya Kisyria na vyama vya siasa katika kile ilichoita ``Mkutano wa Syria katika majadiliano ya Kitaifa``
Rais wa Urusi, Vladmir Putin, kwanza alidokeza wazo la mkutano huo mwezi uliopita na kusema kuwa anaamini Moscow na serikali ya Syria hivi punde itawadhibiti waasi nchini humo.
Akisaidiwa na ndege za Urusi na wanamgambo wa Kishia wanaoungw amkono na Iran, Rais Assad amewadhibiti waasi wa Syria ambao walikuwa wakipigana ili kumpindua, na kumfanya kuwa imara kijeshi na waasi wakisema wamedhibiti maeneo ya magharibi.
Serikali ya Damascus na washirika wake, wameyakomboa maeneo ya kati na mashariki mwa Syria kutoka katika mikono ya IS katika miezi ya hivi karibuni. Wakati huo huo, kampeni nyingine inayofanywa na vikosi vya Kidemokrasia vya Syria vinavyosaidiwa na Marekani(SDF) imewaondoa IS katika maeneo mengine ya nchi hiyo.
Kampeni nyingine tofauti kwa sasa zimekusanyika katika ngome kuu za IS; katika jimbo la Deir al-Zor mpakani mwa Iraq. Uamuzi wa Urusi wa kualika makundi ya Kikurd yanayodhibiti kundi la SDF kwa mkutano wa Sochi, ulichochea hasira za Waturuki Jumanne.
Serikali ya mjini Ankara ambayo inayaona Makundi makubwa ya Kikurdi ya Syria kuwa ni tishio la usalama wa nchi, imesema haikubaliki kwamba majeshi ya Kikurdi ya YPG; yamealikwa.
Msemaji wa rais wa Uturuki, Ibrahim Kalin amesema maofisa wa Uturuki na wa Urusi, wamejadili suala hilo na kuwa amefanya mkutano wake ili kutatua shida hiyo mara moja.
Uturuki inaona kuwa kundi la YPG na washirika wake wa kisiasa, PYD; ni kama tawi la kundi la chama cha wafanyakati vya Kikurdi, ambalo limekuwa likiendeleza vurugu kwa miongo mitatu nchini Uturuki.
MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.
Maoni