MTEULE THE BEST Image caption Alexi Sanchez Arsenal wamempa Alexis Sanchez mkataba mpya na mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL. (Daily Mail) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa "hana uhakika sana" kama ataweza kumshawishi Alexis Sanchez kukubali kusaini mkataba mpya. (SFR) Juventus wanajiandaa kutoa pauni milioni 23 kujaribu kuishawishi Liverpool kumuuza Emre Can. (Gazzetta dello Sports Juventus nao wameingia katika mbio za kutaka kumsajili Sergi Roberto kutoka Barcelona, ambaye pia Manchester United na Chelsea zinamtaka. (Sport.es) West Ham wamepanda dau la pauni milioni 27.1 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25. (Daily Telegraph) Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Liverpool hawataki kumuuza Philippe Coutinho kwa Barcelona Barcelona hawatakuwa na uwezo wa kumnunua Philippe Coutinho kutoka Liverpool iwapo watafanikiwa kumsajili Ousmane Dembele, 20, kutoka Borussia Dortmund,...