MTEULE THE BEST
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China amemuambia mwenzake wa Korea Kaskazini kuwa Korea Kaskazini itahitaji kusitisha majaribio ya makombora baada ya vikwazo vipya vilivyowekwa na baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa.
Wang Yi anasema alimshauri Ri Yong-ho kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wao uliofanyika nchini Ufilipino.
Hata hivyo hakusema vile bwana Ri alijibu.
Siku ya Jumamosi baraza la usalama la Umoja wa mataifa, lilichukua hatua madhubuti ya kuiadhibu Korea Kaskazini kwa hatua yake ya mwezi uliopita ya kuifanyia majaribio zana zake za kitonoradi.
Katika kura ya pamoja, baraza hilo liliidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe ya Pyongyang ambayo huuza nje bidhaa hizo kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.
Rais wa Marekani Donald Trump, alipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la Umoja wa mataifa.
Anasema kuwa, vikwazo hivyo, vitakuwa na "athari kubwa mno" ya kibiashara.
Majirani wao Korea Kusini, wameiomba Korea Kaskazini kufuata njia ya mazungumzo, ili kutanzua mzozo uliopo wa mpango wa Pyongyang, kuhusu zana za kinuklia.
Beijing pia inaomba kurejelewa kwa mazungumzo
Maoni