Tamko la Marekani na Uingereza linagusia kesi ya Erick Kabendera kama mfano wa hivi karibuni Ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania." Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria. "Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo. "Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria k...