Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SIRAHA

RAIS APINGANA NA UAMUZI WA BUNGE

Trump akaidi uamuzi wa bunge na kuamua kuiuzuia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya $8bn Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia Rais huyo wa Marekani ametumia kura ya turufu kufutilia mbali uamuzi wa bunge la Congress la kuzuia mauzo ya silaha yenye thamani ya $8bn kwa Saudia na UAE. Donald Trump alisema kuwa maamuzi hayo matatu yatadhoofisha uwezo wa Marekani ulimwenguni na kuharibu uhusiano wake na washirika wake . Hatua hiyo inajiri baada ya mabunge yote mawili kupiga kura ya kuzuia mauzo hayo. Baadhi ya wabunge wanasema kwamba walihofia kwamba silaha hizo huenda zikatumiwa dhidi ya raia katika mgogoro wa Yemen. Wameshutumu vitendo vya Saudia nchini Yemen pamoja na mauaji ya mwaka jana ya mwandishi Jamal Khashoggi. Hatahivyo bunge le seneti litapiga kura baada ya siku moja ili kuona iwapo litakaidi uamuzi wa bwana Trump , kulingana na kiongozi wa wengi katika chama cha Republican Mitch Connel. Lakin...

Iran 'imeongeza urutubishaji wa uranium' baada ya vikwazo vya Marekani

inu cha Bushehr kinaweza kutumia madini ya uranium kama nishati Iran imekiuka makubalino ya kiwango inachopaswa kurutubisha cha madini ya uranium kwa mujibu wa mkataba wa 2015 ulioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani, vyombo vya habari Iran vinaripoti. Shirika la habari la Isna limemnukuu waziri wa mambo ya nje nchini humo aliyethibitisha kuwa taifa hilo limerutubisha zaidi ya kilo 300 zilizotakiwa Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki limesema litwasilisha ripoti. Iran imeshinikiza urutubishaji huo wa uranium inayotumika kama nishati na pia silaha za nyuklia kufuatia kuidhinishwa upya vikwazo vya marekani dhidi yake. Mataifa ya Ulaya yameonya kuwa ukiukaji wowote utakuwa na athari zake. Je Marekani ina malengo gani Iran? Je unayafahamu yaliomo katika mkataba wa nyukilia wa Iran ? Trump ajibu kauli ya Iran aliyoiita ya ''kijinga na yenye matusi'' Iwapo hilo litathibitishwa na shirika la IAEA, linatoa fursa kuidhinishwa upya kwa vikwazo vili...

Maandamano Sudan: Vikosi vya jeshi vyazozana Khartoum

Baadhi ya wanajeshi wameanza kuwalinda waaandamanaji mjini Lkhartoum baada ya vikosi vya usalama kurusha vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kulingana na mashahidi. Wanajeshi walionekana wakijaribu kuyafukuza magari yaliokuwa yakijaribu kurusha vitoa machozi katika siku ya pili ya maandamano ya kutaka rais Omar al-Bashir kung'atuka uongozini. Waandamanaji walionekana wakitafuta hifadhi katika kifaa cha jeshi la wanamaji huku wasiwasi kati ya majeshi ukioonekana wazi. Bashir kufikia sasa amekataa kuondoka mamlakani ili kutoa fursa kwa serikali ya mpito. Maelfu ya waandamanaji wamekita kambi nje ya makao makuu ya jeshi nchini Sudan, wakimtaka rais Omar al-Bashir ajiuzulu. Inavyoonekana wanatarajia mapinduzi ya ndani ya nchi, wakiliomba jeshi kumtimua Bashir na kufungua njia ya kupatikana serikali ya mpito. Ni maandamano makubwa dhidi ya Bashir tangu kuzuka ghasia mnamo Desemba mwaka jana. Bashir amekataa kuondoka, akieleza kwamba wapinzani wake wanastahili kutafuta u...

Rais Vladimir Putin amesema Urusi itaanza kuunda makombora mapya

  Marekani inahofia makombora mapyaya Urusi Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi sawa na huo uliyochukuliwa na Marekani. Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya. Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake siku ya Ijumaa. Mkataba huo uliyofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri. "Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi. Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya magharibi Nato, Jens Stoltenberg amaiambia kuwa: "Washirika wote [Ulaya] yameunga mkono hatua ya Marekani kwasababu Ur...

Vladimir Putin asema Urusi ina kombora lisiloweza kuzuiwa

Haki miliki ya picha AFP Image caption Ilikuwa hotuba ya mwisho kwa Bw Putin kabla ya uchaguzi Urusi imeunda kombora jipya ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin. Bw Putin amekuwa akieleza sera zake muhimu za muhula wa nne, taifa hilo linapokaribia kufanya uchaguzi katika siku 17. Rais huyo anatarajiwa kushinda. Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale. Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo." Katika nusu ya kwanza ya hotuba hiyo yake kwa taifa, ameahidi kupunguza viwango vya umaskini nchini humo. Kisha, ameonesha mkusanyiko wa silaha mpya, likiwemo kombora alilosema linaweza "kufika pahala popote duniani". Hotuba hiyo ya Bw Putin imeendelea kw...