Marekani inahofia makombora mapyaya Urusi
Urusi imejiondoa katika mkataba wa kupinga uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa enzi ya vita baridi kufutia uamuzi sawa na huo uliyochukuliwa na Marekani.
Rais Vladimir Putin amesema taifa hilo litaanza kuunda makombora mapya.
Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba huo ilitangaza kusitisha rasmi wajibu wake siku ya Ijumaa.
Mkataba huo uliyofikiwa kati ya Marekani na muungano wa Sovieti, USSR na kutiwa saini mwaka 1987 ulipiga marufuku mataifa yote dhidi ya matumizi ya makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.
"Washirika wetu wa Marekani wametangaza kusitisha wajibu wao katika mkataba huo nasi pia tunafuata mkondo wao,"alisema Bw. Putin siku ya Jumamosi.
Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi
Katibu mkuu wa muungano wa kijeshi wa mataifa ya magharibi Nato, Jens Stoltenberg amaiambia kuwa: "Washirika wote [Ulaya] yameunga mkono hatua ya Marekani kwasababu Urusi imekiuka mkataba huo kwa miaka kadhaa."
Alisema makataa ya miezi sita iliyotolewa na Marekani kwa Urusi kufuata kutekeleza kikamilifu yanafaa kuzingatiwa.
Urusi imekuwa ikikanusha tuhuma za kukiuka mkataba wa vita baridi.
Rais wa Putin aidha amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Urusi inalaumiwa kwa nini?
Marekani imesema ina ushahidi kuwa kombora mpya iliyoundwa na Urusi ni moja ya mokombora yaliyopigwa marufuku katika mkataba wa INF.
Baadhi ya maafisa wa Marekani wanasema kuwa makombora ya aina ya 9M729 - yanayotambuilwa na Nato kama SSC-8 tayari yameanza kutumika.
Mwezi Disemba mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump, aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba wa INF ikiwa Urusi haitabadili msimamo wake.
Kombora mpya aina 9M729 lililoundwa na Urusi inatia Marekani tumbo joto
Nini kitakachofuata?
Katika mkutano wa Jumamosi akiandamana na mawaziri wake ulinzi na wa mambo ya nje, rais Putin alisema wataanza kuunda silaha mpya ikiwa ni pamoja na makombora ya kulipua meli na mengine yaliyo na kasi ya mara tano zaidi ya mlio wasauti.
Bw. Putin hata hivyo amesema kuwa hatajihusisha katika mradi wa gharama ya juu ya uundaji silaha na kuongeza kuwa taifa lake litatumia silaha hizo endapo marekani itaanza kuzitumia.
''Mashindano ya uundaji wa silaha kama hizo ni tishio kubwa kwa mataifa ya bara Ulaya'' Jens Stoltenberg aliiambia BBC .
Ni yapi yaliyomo katika makubaliano ya kuunda makombora ya masafa ya kadri (INF)?
Kiongozi wa Sovieti Mikhail Gorbachev na rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan walitia saini mkataba wa INF mwaka 1987
Mkataba huo uliotiwa saini na Marekani na USSR mwaka in 1987, ulikuwa wa kudhibiti uundaji wa silaha za nuklia na makombora ya masafa ya mafupi na ya kadri, isipokuwa yale ya kurushwa baharini.
Marekani ilikuwa na hofu kuhusiana hatua ya Usoviyeti kuunda kombora la USS-20 na kujibu hatua hiyo kwa kuunda makombora ya kulipua meli barani Ulaya - hatua hiyo ililaaniwa sana.
Kufikia mwaka 1991, karibu makombora 2,700 ilikuwa imeharibiwa.
Mataifa yote mawili yaliruhusiwa kukagua mitambo ya mwingine.
Mwaka 2007, rais wa Urusi Vladimir Putin ilitangaza kuwa mkataba huo haulindi tena maslahi yake
Hatua hiyo ilikuja baada ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa marefu uliyofikiwa mwaka 2002
Mara ya mwisho Marekani ilijiondoa katika mkataba wa silaha ilikuwa mwaka 2002, wakati rais George W Bush alipojiondoa kutoka mkataba wa kudhibiti uundaji wa makombora ya nuklia ambayo ilipiga marufuku uundaji wa silaha za kujibu mahambulio ya silaha hizo.
'
Hatua ya utawala wake wa kuweka kituo cha kujikinga dhidi ya makombora barani ulaya iliikasirisha Kremlin.
Hata hivyo kituo hicho kilifungwa na utawala wa Obama mwaka 2009 na mahala pake pakachukuliwa na mfumo wa ulinzi uliyoimarishwa mwaka 2016
Maoni