Airbus A220-300: Ndege mpya ambayo imenunuliwa na Tanzania imewasili Dar es Salaam Airbus A220-300: Ndege mpya ambayo imenunuliwa na Tanzania imewasili Dar es Salaam Ndege mpya ambayo imekuwa ya karibuni zaidi kununuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania imewasili Dar es Salaam. Ndege hiyo, ambayo imeundwa na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus, ni ya muundo wa A220-300. Ndege hiyo itakuwa na jina la Dodoma, mji mkuu rasmi wa Tanzania. Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa kuhamishia shughuli zake zote jijini Dodoma. Tanzania iliponunua ndege ya majuzi zaidi, 787-8 Dreamliner ya kampuni ya Boeing, ndege hiyo ilipewa jina la Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika. Sawa na ndege hiyo ya Dreamliner, ndege hiyo mpya ya Airbus ina nembo ya 'Hapa Kazi Tu' chini ya jina Dodoma. Hapa Kazi Tu imekuwa kauli mbiu ya Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli tangu wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015. Kampuni ya...