Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 11, 2016

Pande pinzani zakubaliana kuhusu mpango wa uchaguzi DRC

MTEULE THE BEST Image copyright GETTY IMAGES Image caption Rais wa DRC Joseph Kabila Wapatanishi katika mazungumzo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa pande husika zimekubali kuhusu mpangilio wa uchaguzi utakavyofanyika,swala ambalo lilifanya upinzani kujiondoa katika meza ya mazungumzo mapema wiki hii. Tuhuma kwamba huenda rais Joseph kabila akajaribu kujiongezea muda wa kutawala baada ya muhula wake wa pili kukamilika imesababisha mgogoro wa kisiasa nchini humo. Waziri wa haki Alexis Thambwe Mwamba amesema kuwa chini ya makubaliano hayo ambayo hayajatiwa saini,uchaguzi wa urais,ule wa kitaifa pamoja na ule wa kijimbo itafanyika siku moja. Bwana Mwamba ameongezea kwa serikali ya mda ikishirikisha wanachama wa upinzani itabuniwa ili kusaidia kutatua mgogoro huo wa uchaguzi. Makundi mengi ya upinzani yamesusia mazungumzo hayo ili kutohalalisha mchakato wa mazungumzo hayo. Mapema shirika la Amnesty International lilichapisha ripoti ambayo ilishtumu mamlaka ya...

Juncker aitaka Ulaya kuunda jeshi la pamoja

MTEULE THE BEST Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean- Claude Juncker amefichua mapendekezo kadhaa ya kufufua hali ya uaminifu unaoporomoka wa Umoja huo baada ya kura ya Uingereza ya kujitoa katika umoja huo ya Brexit. Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker akihutubia bunge la Ulaya Mapendekezo hayo ni pamoja na makao makuu mapya ya ulinzi na pia utengenezaji wa nafasi za kazi pamoja na kuimarisha ukaguzi wa mipaka. Juncker amewtoa wito wa kuanzisha makao makuu ya jeshi la Umoja wa ulaya ili kuratibu juhudi kuelekea kuunda jeshi la pamoja ambapo baadhi ya mali zake zinamilikiwa na Umoja wa Ulaya. Lakini alisisitiza kwamba mipango hiyo haitachafua mahusiano na Jumuiya ya NATO, ambayo ina wanachama wengi ndani ya Umoja huo. Bunge la Ulaya mjini Straßburg Uingereza , ambayo ilipiga kura kujitoa kutoka Umoja huo Juni 23 , hapo kabla ilipinga vikali hatua zozote kuelekea kuwa na jeshi la pamoja la Umoja wa Ulaya. Juncker pia alishauri kumfanya ...

Merkel ataka wakimbizi waajiriwe

MTEULE THE BEST Kansela wa Ujeruamni Angela Merkel amesema Ujerumani inahitaji suluhisho madhubuti kuwajumuisha wakimbizi katika soko la ajira la Ujerumani kama nguvu kazi. Merkel aliyasema hayo baada ya kukutana na kampuni mbalimbali. Katika juhudi za kuyatetea maisha yake katika siasa, Bi Merkel aliwaita wakuu wa baadhi ya kampuni kubwa kabisa za Ujerumani kwa ajili ya mkutano mjini Frankfurt kufafanua kwa nini hawajachukua hatua kuwapa ajira wakimbizi na pia kubadilishana mawazo kuhusu jinsi wanavyoweza kushirikiana. Kampuni nyingi zinahoji kwamba ukosefu wa ujuzi wa lugha ya Kijerumani, wakimbizi wengi kushindwa kuthibitisha wana sifa au vigezo na pia kukosekana uhakika wa wao kuendelee kuishi Ujerumani, ina maana hakuna mengi ambayo kampuni hizo zinaweza kuyafanya katika kipindi kifupi. Kansela Merkel ameiambia radio ya rbb-inforadio kwamba ikihitajika, mazingira maalumu yanaweza yakaandaliwa kuharakisha mchakato wa kuwajumuisha wakimbizi katika soko la ajira, laki...

Choo kilichotengezwa kwa dhahabu kutumika na umma

MTEULE THE BEST Image caption Choo kilichotengezwa na dhahabu Raia wako huru kutumia fedha zao kidogo ili kupata huduma ya choo kilichotengezwa na dhahabu katika jumba la makumbusho la Guggenheim. Msanii kutoka Italy,Maurizio Cattelan alijenga choo hicho kwa kutumia carat 18 za dhahabu na kukiita choo hicho Marekani. Choo hicho cha maonyesho kimewekwa katika msala wa kuogea wa Guggenheim kulingana na the New Yorker. Image caption Msanii Maurizo Cattelan kutoka Italy Jumba hilo la makumbusho limekitaja choo hicho kuwa kazi nzuri. Choo hicho cha dhahabu kilijengwa katika choo chengine kinachotumiwa na jinsia zote mbili. Wageni wanaolipa kiingilio cha jumba hilo la makumbusho wataweza kukitumia wanavyotaka. Image copyright TWITTER Image caption Choo kilichotengezwa na dhahabu Choo hicho kinalenga kuwapa fursa raia wa tabaka la chini kujifurahisha katika mandhari ambayo hutumiwa na matajiri pekee

Malori ya Kenya na Tanzania yachomwa moto DRC

MTEULE THE BEST   Magari 13 ya mizigo yanayotoka Tanzania na Kenya yamechomwa moto Image caption Ramani ya taifa la DRC katika vijiji vya Kasebebena na Matete kilometa 30 kutoka mji wa Namoya katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania,Mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics inayomiliki magari 10 kati ya yaliyopata kadhia hiyo, Azim Dewji amesema magari yake manne yameteketea kabisa na mengine sita yameungua Image copyright TWITTER Image caption Chapisho la mtandao wa Twitter wa msemaji wa serikali ya Tanzania kidogo huku magari mengine matatu kutoka Kenya nayo yakiteketea kabisa. Gazeti hilo linadai kuwa,Dewji amesema madereva wa magari hayo walitekwa huku wakipewa sharti la kutaka majeshi ya Tanzania yaliyo katika ulinzi wa amani nchini humo yaondoke ili wawaachilie. Image copyright TWITTER Image caption Chapisho la mtandao wa Twitter wa msemaji wa serikali ya Tanzania Mwananchi linasema kuwa ,hata hi...

Mabaki yaliyopatikana Pemba, Tanzania ni ya MH370

MTEULE THE BEST Image copyright SERIKALI, TANZANIA Mabaki ya ndege yaliyopatikana katika pwani ya visiwa vya Pemba nchini Tanzania yalitoka kwa ndege ya shirika la Malaysia Airlines iliyotoweka mwaka 2014, maafisa wa Malaysia wamethibitisha. Waziri wa uchukuzi wa Malaysia Liow Tiong Lai amesema kupitia taarifa, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kwamba baada ya uchunguzi imebainika kwamba kipande hicho kikubwa cha bati kilichopatikana mwezi Juni ni cha ndege hiyo safari nambari MH370. Amesema uamuzi huo ulifikiwa na wataalamu kutoka Idara ya Usalama wa Safari za Ndege ya Australia (ATSB) na wale wa kuchunguza usalama wa MH370. Mapema Julai, waziri wa uchukuzi wa Australia Darren Chester alikuwa amedokeza kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa mabaki hayo yalikuwa ya ndege hiyo. Alisema muundo wa mabaki hayo, ukubwa wake na muonekano wake viliashiria kwamba yalikuwa ya ndege hiyo ya Malaysia. Mabaki hayo pia yalikuwa na muhuri wa kuonesha tarehe ya kuundwa kwake ...