Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 26.07.2019: Zaha, Maguire, Bale, Pogba, Neymar, Malcom Manchester United huenda ikalazimika kulipa Leicester City £80m kumnunua mlinzi wake Harry Maguire baada ya Eric Bailly kuumia goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham. (Mirror) Winga wa Leicester Muingereza Demarai Gray 23- amesema hakuna haja ya kuwa na "hofu" kuhusu uhamisho wa Maguire na kuongeza kuwa haamini nyota huyo wa miaka, 26, ana msongo wa mawazo kuhusu hatma yake. (Leicester Mercury) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai kuwa wanamlenga mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na kusisitiza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kilichopo badala ya kununua wachezaji wapya. (Independent) Gareth Bale alijiunga na Real Madrid mwaka 2013 Everton imeifahamisha Crystal Palace kuwa wanaandaa dao la £60m kumnunua mshambuliiaji wa Uturuki Cenk Tosun kama sehemu ya mkataba wa kumzuilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26 ...