Philippe Coutinho
Winga wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho - ambaye kwa sasa yupo Barcelona ya Uhispania- anasema hana mpango wa kurejea kwenye ligi ya Premia. Coutinho, 26, ambaye ni nyota pia wa timu ya taifa ya Brazil alijiunga na Barca Januari 2018. (Mirror)
Real Madrid wanatarajiwa kutangaza dau la kumnunua kipa wa Chelsea raia wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 24. (Teamtalk)
Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa klabu ya Athletico Paranaense ya nchini Brazil Bruno Guimaraes, 21, iwapo watafamikiwa kuchomoka kwenye marufuku ya kufanya usajili. (Mail)
Real Madrid wanamatumaini kuwa wakala Mino Raiola atamshawishi mchezaji wake Paul Pogba, 26, ahamie timu yao kutoka Manchester United. (Marca)
AC Milan wanamtaka kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino kumrithi Gennaro Gattuso kushika mikoba ya timu hiyo na watampatia kitita cha pauni milioni ili afanye usajili wa wachezaji mwishoni mwa msimu huu. (Mirror)
Kablya ya kutua Spurs, Mauricio Pochettino alikuwa meneja wa Espanyol kati ya 2009 na 2012.
Liverpool wapo tayari kumpa mkataba mpya mshambuliaji raia wa Ubelgiji Divock Origi, 23. (Football Insider)
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anaamini kuwa mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Olivier Giroud, 32, ataendelea kusalia klabuni hapo msimu ujao. (Mail)
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri
Kocha wa West Ham Manuel Pellegrini anataka kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Roma na timu ya taifa ya Bosnia Edin Dzeko, 33. (Express)
Kipa wa zamani wa taifa la Uholanzi Edwin van der Sar amesema "siku moja" anaweza kurejea Manchester United. Mkongwe huyo mwenye miaka 48, kwa sasa ni mkurugenzi wa mpira wa miguu kwenye klabu ya Ajax, na enzi zake aliichezea United kwa misimu sita. (Times - subscription required
Maoni