Raia watakaondamana kwa lengo la kuwashinikiza wabunge kushirikiana na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG nchini Tanzania watakiona cha mtema kuni.
Onyo hilo limetoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ambaye amewatahadharisha waliopanga maandamano hayo hapo siku ya Jumanne kwamba watapigwa hadi ''kuchakaa''.
Afisa huyo amesema kwamba baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kulishinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.
Muroto ameonya kuwa wale wanaopanaga kufanya safari kuelekea mjini Dodoma ili kushiriki katika maandamano hayo wataambulia kupigwa na kuchakaa.
''Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," amesema Muroto.
Afisa huyo amesisitiza kuwa maswala ya bunge hutekelezwa ndani ya bunge na wala sio nje hivyobasi akawaomba wananchi wa Dodoma kuendelea na kazi zao kama kawaida kwani hakuna maandamano yoyote yatakayofanyika.
YoungGalaxy@YoungMkurujenzi
#IStandWithCAG #I stand with Prof Assad@zittokabwe @KumbushoDawson @MariaSTsehai
1
See YoungGalaxy's other Tweets
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @YoungMkurujenzi
Ameongezea kuwa jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na wale wote watakaoshirki katika maandamano hayo
Mnamo tarehe mbili mwezi huu, Bunge la Tanzania liliazimia kutofanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali, (CAG) wa nchi hiyo Prof Musa Assad baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za dharau kwa chombo hicho.
Wabunge waliafikia uamuzi huo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutaka waridhie mapendekezo yao dhidi ya CAG.
Kamati hiyo ilimhoji CAG Januari 21 baada ya kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York mwezi Disemba 2018 ambapo alisema kuwa Bunge la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali.
Spika Job Ndugai alilieleza Bunge mwezi Januari kuwa maelezo ya Assad yalioonesha dharau kubwa dhidi ya mhimili huo na kumtaka aende mbele ya kamati kwa hiyari yake, ama apelekwe kwa pingu.
Hatahivyo Profesa Mussa Assad wiki iliopita akizungumzia mgogoro baina yake na Bunge alisema unaweza kuzaa mgogoro wa kikatiba.
Bunge la Tanzania lilipitisha azimio la kutokufanya kazi na CAG baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za kudharau chombo hicho.
Wabunge wamefikia uamuzi huo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutaka waridhie mapendekezo yao dhidi ya CAG.
Zitto Kabwe Ruyagwa
✔@zittokabwe
All this to threaten young people who demands that constitution be respected RE: parliament v Auditor General? Number one duty of armed forces is to PROTECT the constitutional order. Anyways, @tanpol will be happier with a weak CAG because of their corrupt deals
317
108 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
Profesa Assad amenukuliwa akisema kuwa suala hilo linaweza kuwa kubwa kuliko lilivyo sasa. Prof Assad ametoa rai kuwa busara itumike zaidi ili kupata ufumbuzi.
"Tunaweza kuwa na mgogoro wa kikatiba, kwamba ripoti (za ukaguzi wa mwaka 2017-18) zimeshawasilishwa kwa Raisi na mimi siwakilishi ripoti Bungeni, basi raisi atazipeleka ndani ya siku sita zijazo na kama Bunge likikataa kuzipokea hiyo ni tatizo kubwa zaidi. Ni dharau (kwa katiba)wasiwasi wangu ni huo. Zikiwasilishwa bungeni zinakuwa mali ya umma na mimi napata nafasi ya kuzungumza, na hilo pia linaweza kuwa tatizo. Tafsiri ya kuwa (Bunge) hatuwezi kufanya kazi na CAG ni tafsiri pana sana na inatakiwa tuijue vizuri," amesema Prof Assad.
Alipoulizwa endapo anaweza kuchukua 'uamuzi mgumu' , Prof Assad amesema, "hana maamuzi ya kufanya zaidi ya kuomba dua watu waongoze vizuri na wafanye maamuzi yenye faida na nchi hii, basi."
Prof Assad amesema pia ataendelea kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa kwenye katiba.
The Citizen Tanzania@TheCitizenTZ
CAG, Parliament tussle could weaken transparency, accountability, Wajibu warns http://bit.ly/2K9Oken
5
See The Citizen Tanzania's other Tweets
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @TheCitizenTZ
Kitengo cha vijana katika chama cha upinzani cha ACT kimepanga kufanya maandamano hapo kesho kulishinikiza bunge kufutilia mbali azimio lake la kutoshirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.
Kulingana na Katibu wa Mawasiliano katika chama hicho kitengo cha vijana Karama Kaila, watafanya maandamano kulishinikiza bunge kupokea taarifa za CAG zikiwa na saini ya Profesa Assad ifikiapo tarehe 10 mwezi Aprili.
What next as Tanzanian MPs refuse to work with CAG? - The East African http://dlvr.it/R2KTPwWhat next as Tanzanian MPs refuse to work with CAG?
The Auditor General described the parliament as 'too weak' to hold the government accountable.
theeastafrican.co.ke
See Tanzania tours's other Tweets
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @Tanzania_tours_
Kumbusho Dawson Kagine@KumbushoDawson
More than 13,000 people have signed an online petition launched to pressure Tanzania’s Parliament to rescind its recent resolution against the Controller and Auditor General (CAG), Prof Mussa Assad. https://www.changetanzania.org/petitions/ #IStandWithCAG #ChangeTanzania
79
25 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @KumbushoDawson
Amesema watashirikiana na vijana wa vyama vya kisiasa vya NCCR Mageuzi, CHAUMA, UPDP na vyama vingine vitatu kfufanya maandamano hayo ya amani mkoani Dodoma siku hiyo.
"Tumefikia uamuzi huu baada ya kujiridhisha kwamba uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na Bunge kwa ujumla wake kusitisha kufanya kazi na CAG ni kinyume na Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambayo imeanzisha Mamlaka ya CAG na kuzuia kabisa kuingiliwa katika majukumu yake na kwamba ni wajibu wa kila raia kuilinda Katiba," amesema Kaila.
Maoni