Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MISRI

Fedha za ndani kugharamia mradi wa kufua umeme

Fedha za ndani kugharamia mradi wa kufua umeme wa kilowati 2115 Raisi wa Tanzania Dokta John Magufuli akisalimiana na Waziri wa nishati wa Misri Dokta Mohamed Shaker Raisi John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto Rufiji utakaozalisha umeme wa kilowati 2115 Mradi huu utakaogharimu kiasi cha trilioni 6.5 za Tanzania, zikiwa fedha za ndani, ulipangwa kutekelezwa kwa miezi 42 hivi sasa ikiwa imebaki miezi 36 pekee ili kuukamilisha, Umeme utakaozalishwa utasafirishwa kutoka Rufiji kuelekea Chalinze , umbali wa km 167 kisha Dar es Salaam na Dodoma pia umeme utakaozalishwa utaweza kuendesha treni za mwendo kasi. Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Dokta Medard Kalemani amesema malengo ya serikali ni kuzalisha umeme wa megawatt 10000 ifikapo mwaka 2025. Mradi huu una manufaa gani? Utasaidia udhibiti uharibifu wa mazingira, Dar es Salaam pekee magunia laki 5 ya mkaa hupelekwa na kutumika kila mwezi kutoka msituni, Asilimia 71.2 ya watanz...

Mamlaka nchini Kenya zawazuia marubani wanafunzi kutua nchini humo

Marubani wanafunzi wa Afrika Kusini, waliotengeneza ndege aina ya Sling 4, wamewasili Kilimanjaro,Tanzania, wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo chao cha mwisho, jijini Cairo. Timu ya wanafunzi hao waliondoka Zanzibar siku ya Jumapili, baada ya kutumia siku kadhaa bila mafanikio kuzungumza na mamlaka za nchini Kenya ili waweze kutua jijini Nairobi. ''Mamlaka nchini Kenya wamesema hawajafurahishwa na njia zetu hivyo wakatuzuia kuingia,'' alisema kiongozi wa wanafunzi hao, Des Werner, Baba wa Megan Werner 17, mwanzilishi waU-Dream Global. ''Tunaweza kubadili njia lakini hatuna muda wa kufanya hivyo.Tunafikiri kama ni wagumu tusilazimishe kwenda. Hata hivyo ni nchi yao ndio inayokosa nafasi ya vijana wa nchini kwao kuzungumza na timu yetu kwa ajili ya kuwapa msukumo vijana wa nchini mwao.'' Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi yatua Zanzibar Wanafunzi kuendesha ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Misri Marubani hao wataelekea Uganda siku ya Jumanne l...

AFCON: CAF YA TANGAZA BEI ZA KUONA MCHEZO HUKO MISRI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali za Africa (AFCON) zinazotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri. Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliyebebwa na wachezaji. Shrikisho la soka nchini TFF limethibitisha taarifa hiyo, ikisema kuwa CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali. Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la kwanza ni USD 29 ambayo ni sawa na takribani sh 66,700 za Kitanzania, tiketi za daraja la pili ni USD 18 ambazo ni sawa na sh 41,403 tiketi za daraja la tatu ni USD 6. Katika hatua ya makundi, Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja la kwanza ni  USD 35 ambayo ni takribani sh 80,521 kwa daraja la pili ni USD 24 na daraja la tatu ni ...

Vilabu bingwa Afrika: Droo ya Total CAF Confederation Cup

S imba ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya zapewa wapinzani Droo ya kombe la Vilabu bingwa barani Afrika hatimaye imetolewa. Katika michuano hiyo klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa wa zamani wa kombe hilo TP Mazembe wa DR Congo huku mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia wakimenyana dhidi ya klabu ya S Berkane kutoka Morocco. Droo hiyo iliofanyika siku ya Jumatano katika mji wa mkuu wa Misri, Cairo iliwakutanisha mabingwa hao huku safari ya michuano hiyo ikielekea kufika ukingoni. Baadhi ya magwiji wa kandanda waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CAF Anthony Baffoe, chini ya usaidizi wa mshambuliaji wa zamani wa Cameroon Patrick Mboma pamoja na Emad Moteab kutoka Misri. Pia baadhi ya waliohudhuria walikuwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki. Jinsi Simba na Gor  M ahia zilivyotinga robo fainali Katika hatua ya kuelekea robo fainali klabu ya Simba ya Tanzania ilivunja mwiko wa miaka 25 baada ya kuilaza klabu ya Vit...