Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AUSTRIA

Austria imerudi katika utawala wa mrengo wa kulia

MTEULE THE BEST Sebastian Kurz (kulia) na Heinz-Christian Strache wa Freedom Party Austria inakuwa nchi pekee ya Uropa magharibi kuwa na chama tawala kilicho na misimamo mikali ya mrengo wa kulia Rais wa Austria, Alexander Van der Bellen ameidhinisha kuundwa serikali ya muungano kati ya chama cha kihafidhina People's Party na cha mrengo wa kulia Freedom Party. Austria inaelekea kuwa nchi pekee ya Uropa magharibi kuwa na chama tawala kilicho na misimamo mikali ya mrengo wa kulia. Hii inatokana na hatua ya kiongozi Sebastian Kurz wa chama cha conservative Austrian People's Party kuridhia ushirikiano na chama kidogo cha mrengo wa kulia Freedom Party kinachoongozwa na Heinz-Christian Strache, ambao wao wanaendeleza sera kali hasa dhidi ya wahamiaji. Bwana Kurz mwenye ana miaka 31 pekee, na kama mpango huu utafanikiwa atakuwa pia kiongozi wa serikali mwenye umri mdogo zaidi duniani. Kwa muda wa miezi miwili sasa bunge la nchi hiyo limekuwa likijadili vipi kuzuia u...