Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 4, 2026

WANANCHI DAR ES SALAAM WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUCHUNGUZA MABUSHA

Picha
Wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa Jirani wamehimizwa kujitokeza kuchunguza Mabusha na kupata huduma bure ya upasuaji wa ugonjwa huo. Rai hiyo imetolewa leo Januari 8 ,2026 na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Mhe. Albert Chalamila Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kambi ya Upasuaji wa Mabusha iliyoanza tarehe 5 hadi 30 Januari, 2026. "Nitoe rai kwa Wananchi wa Dar es Salaam na mikoa jirani kujitokeza kuchunguza afya zao hasa uchunguzi wa Mabusha na endapo atabainika matibabu yanatolewa bila malipo yanagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 na lengo ni kufanya upasuaji wa Mabusha kwa zaidi ya Wananchi 500" amesema Mhe. Mtambule Kwa upande wake Mganga Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Mohammed Manuna amesema hadi sasa jumla ya Wananchi 165 wamefanyiwa uchunguzi wa Mabusha huku 127 wakibainika na tatizo hilo na 27 wakiwa tayari wameshafanyiwa huduma ya upasuaji. "Karibu asilimia moja ya wagonj...