Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 17, 2017

Seneta wa Republican ampinga Trump kuhusu Obamacare

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Bima ya wagonjwa iliyoanzishwa na Rais Barack Obama ijulikanayo kama ObamaCare inawahudumia Wamerakani wa kipato cha chini. Seneta wa chama cha Republican aliyekuwa wakati mmoja mgombeaji wa Urais, John McCain, amesema kuwa atapiga kura kupinga mpango wa chama chake wa kufutilia mbali bima ya wagonjwa iliyoanzishwa na Rais Barack Obama ijulikanayo kama ObamaCare. Alisema kuwa moyo wake haumruhusu kuunga mkoto upigaji marufuku wa bima hiyo inayowasaidia watu wa mapato ya chini bila kuwa na takwimu za kuonyesha watakaonufaika na watakaoathirika. Mbali na Bwana McCain, seneta mwingine mmoja wa Republican amesema kuwa anapinga ufutiliaji mbali wa bima hiyo. Tayari wengine wawili wametangaza kuwa wanapinga mswada huo wa chama cha Republican. Image caption Seneta John McCain wa Republican Kwa kuwa vyama vikuu viwili katika bunge la Seneti linashindiana wanachama wachache sana ni dhah...

Tetemeko la ardhi lasikika Korea Kaskazini, Je ni jaribio la kombora?

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Image caption Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini. Tetemeko hilo lilitokea kilomita 50 kutoka kituo cha majaribio ya makombora ya kinyuklia . Mitetemeko mengine ya ardhi imetokea wakati wa majaribio ya makombora. Wataalam wa mitetemeko nchini China wamesema kuwa wanatuhumu ulikuwa mlipuko. Lakini Korea Kusini inasema kuwa huenda ni tetemeko la kawaida ambalo halikusababishwa na jaribio la kombora la kinyuklia. Korea Kaskazini ilifanya majaribio makubwa ya kombora lake la kinyuklia mnamo Septemba 3 ambalo limeshutumiwa pakubwa katika mkutano wa umoja wa mataifa. Kiwango cha tetemeko la siku ya Jumamosi ni kidogo ikilinganishwa na wakati taifa la Korea Kaskazini linapofanyia majaribio makombora yake.

Rais Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 422 wa jeshi

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha IKULU YA RAIS TANZANIA Image caption Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua paredi ya maafisa wapya kundi la 61/16 kabla ya kuwatunuku kamisheni kuwa maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa shekhe Amri Abeid Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wapya 422 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Maafisa hao wametunukiwa cheo cha Luteni Usu ambapo 314 kati yao walihitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Mkoani Arusha, 84 wakihitimu mafunzo katika shule ya ubaharia ya kijeshi, 14 wakiwa wamehitimu mafunzo katika shule ya urubani ya kijeshi na 10 wakiwa wameiitimu mafunzo ya kijeshi nje ya nchi. Akizungumza baada ya kuwatunuku kamisheni hizo rais Magufuli amewapongeza maafisa hao na kuwataka kuendelea kulitumia Taifa kwa kuzingatia kiapo chao. Amesema kuwa jeshi la ulinzi limefanya kazi kub...

Iran yafanyia majaribio kombora lake

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Image caption Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr. Iran inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la Khorram-shahr. Kombora hilo lilionyeshwa hadharani katika maonyesha ya kijeshi jana Ijumaa. Iran imesema kuwa kombora hilo linaweza kusafiri mwendo wa kilomita 2,000. Marekani yaiwekea Iran vikwazo Ahmadinejad azuiwa kuwania urais Iran Marekani yasikitishwa raia wake kuhukumiwa Iran Iran yaitahadharisha Marekani kuhusu vikwazo Kituo cha runinga cha taifa hilo kilionyesha picha za sherehe hizo. Kombora la kwanza la Khorram-Shahr lilirushwa angani Januari lakini likalipuka katikati ya mwendo. Image caption Rais Donald Trump na rais Rouhani wa Iran Jaribio hilo lilifanywa siku chache baada ya Rais Trump wa Marekani kushambulia Iran katika hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Rais wa Iran, Hassan Rouhani, ametetea hatua ya taifa lake kuimarisha zana zake kwa lengo la kujitetea. ...

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha ALAMY Image caption Magari ya kubeba mafuta kotoka China Kueleka Korea Kaskazini Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani. Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita. Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Rais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifa Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina. Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kaz...

Merkel, Schulz wakamilishia kampeni nyumbani

MTEULE THE BEST Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mpinzani wake mkuu Martin schulz wamerejea katika majimbo yao ya nyumbani kuhitimisha kampeni kabla ya uchauguzi wa Jumapili, wakiwahimiza Wajerumani kukikataa chama cha AfD. Merkel atakamilisha ratiba ya kampeni yake katika jimbo lake la Merklenburg - Vorpommern lililoko katika pwani ya Baltic siku ya Jumamosi. Lakini mbali na kuongoza wilaya ambako chama cha chake cha Christian Democratic Unioni kinaungwa mkono zaidi, atazitembelea pia wilaya za mji wa Greifswald na kisiwa cha Ruegen ambako chama kinachouchukia Uislamu cha Alternatuve für Deutschland - Chama Mabadala kwa Ujerumani - kilipata mafanikio makubwa katika uchaguzi wa jimbo mwaka uliopita. Msosho demokratik Martin Schulz anakamilishia kampeni zake Aachen, mji wa Magharibi mwa Ujerumani ulioko jirani na mji wake wa kuzaliwa wa Wuerselen. Wasiwasi watawala kuhusu AfD Ingawa chama cha Merkel kina uongozi wa tarakimu mbili kulingana na uchunguzi w...

Trump na Kim Jong-Un waitana ''wenda wazimu

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha EPA Image caption Rais Kim Jong Un na mwenzake wa Donald Trump Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ''na matatizo ya kiakili'' yamempatia motisha zaidi ya kuendelea kutengeza makombora ya taifa lake. Katika taarifa ya kibinafsi isio ya kawaida, bwana Kim amesema kuwa rais Trump ''atalipia kauli'' zake za hotuba ya baraza la Umoja wa mataifa ambapo alionya kuiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujilinda. Bwana Trump naye alijibu akisema kuwa ''mwenda wazimu'' hajawahi kufanyiwa atakachofanyiwa akijaribu. Mataifa hayo mawili wamejibizana kwa kurushiana maneneo makali katika siku za hivi karibuni. Rais Kim alimaliza taarifa yake kwa kusema kwamba atamnyamazisha kiongozi huyo ''aliye na akili punguani'' kwa vita. China ilijibu vita hivyo vya maneno ikionya kuwa hali ni mbaya. '...

Soma Magazeti ya Tanzania leo June 23 2017, Udaku, Michezo na Hardnews

MTEULE THE BEST