Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Rais Magufuli awatunuku kamisheni maafisa 422 wa jeshi

MTEULE THE BEST

Rais John Pombe MagufuliHaki miliki ya pichaIKULU YA RAIS TANZANIA
Image captionRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua paredi ya maafisa wapya kundi la 61/16 kabla ya kuwatunuku kamisheni kuwa maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa shekhe Amri Abeid
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wapya 422 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Maafisa hao wametunukiwa cheo cha Luteni Usu ambapo 314 kati yao walihitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Mkoani Arusha, 84 wakihitimu mafunzo katika shule ya ubaharia ya kijeshi, 14 wakiwa wamehitimu mafunzo katika shule ya urubani ya kijeshi na 10 wakiwa wameiitimu mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.
Akizungumza baada ya kuwatunuku kamisheni hizo rais Magufuli amewapongeza maafisa hao na kuwataka kuendelea kulitumia Taifa kwa kuzingatia kiapo chao.
Amesema kuwa jeshi la ulinzi limefanya kazi kubwa kulinda mipaka na kukabiliana na vitisho mbalimbali huku akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuliboresha ili liwe la kisasa zaidi.
Vilevile rais Magufuli amelipatia ruhusa Jeshi hilo kuajiri askari wapya 3,000 huku akiwataka raia wa taifa hilo kuliunga mkono Jeshi lao.
Rais Magufuli aidha alitumia sherehe hizo kueleza juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya Tano tangu iingie madarakani zikiwa ni pamoja na kukabiliana na wizi na rushwa, kununua ndege 6 kwa lengo la kuimarisha usafiri na utalii, kuanza ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti feki katika utumishi wa umma na kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
Magufuli amewataka wananchi wa eneo la Arusha kuungana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali yake na kujiepusha na ushawishi unaolenga kuvuruga umoja na mshikamano hasa wakati huu ambapo Serikali imeamua kuinua uchumi na kudhibiti mianya iliyosababisha upotevu wa rasilimali za Taifa.
"Ahadi niliyoitoa wakati nawaomba kura bado ipo palepale, nitaendelea kuwatumikia watanzania wote bila kuwabagua.
"Tunataka Tanzania mpya yenye maendeleo, tumechezewa mno, wanatupa viroba wao wanakwenda kuchukua dhahabu, wanatupa viroba wao wanakwenda kuiba almasi, wanatupa viroba wao wanakwenda kuiba Tanzanite, nimesema tumechezewa vya kutosha, ni lazima sasa Watanzania tubadilike, ni lazima kila mahali alipo Mtanzania tuweke maslahi ya Tanzania kwanza, Wakati mwingine ukitaka kuwaibia watu unatumia mbinu ya kuwapumbaza na kuwafanya wagombane wao kwa wao, oooh mimi nipo CHADEMA, mimi nipo CCM, ulipozaliwa wala hukuwa na chama, niwaombe Watanzania tubadilike" alisema rais Magufuli

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...