Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya RC

PAPA FRANCISCO NA MAPADRE WATANZANIA & CDF MABEYO

▪︎Katika picha ni Papa Francisco akiwa na Mapadre watanzania wanaosoma na kufanya utume wako nchini Italia pamoja Na Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ▪︎Ikumbukwe Maaskofu wote nchini Tanzania wako katika ziara ya Kichungaji yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani mjini Vatican tangu May 14 hadi May 21, 2023. ▪︎Pia katika ziara hiyo wameambatana na Mapadre kadhaa akiwemo Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Chesco Msaga C.PP.S Naibu Katibu Mkuu (TEC) bila kumsahau Padre Thomas Kiangio Msimamizi  wa Jimbo Katoliki Tanga. . . RADIO MARIA TANZANIA

Papa Francis amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (86), amelazwa katika hospitali ya Gemelli kutokana na matatizo ya kupumua. Msemaji wa Vatican Matteo Bruni amesema kuwa katika siku za karibuni Kiongozi huyo amekuwa akilalamika kuhusu shida hiyo. Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki imeeleza matokeo ya vipimo kuwa ni tatizo kwenye mfumo wa upumuaji. Aidha Vatican imesisitiza kuwa Papa Francis hana Uviko19. Awali Vatican ilieleza kuwa Kiongozi huyo alipelekwa hospital ili kufanyiwa ukaguzi ambao ulishapangwa. Hata hivyo vyombo vya habari vya Italia vilihoji suala hilo kwani mahojiano ya televisheni aliyotakiwa kufanya Papa jioni ya leo yalifutwa dakika za mwisho.

​Papa Francis azungumza juu ya "itikadi ya jinsia"

Papa Francis alikariri upinzani wake dhidi ya watu waliobadili jinsia siku ya Ijumaa, akionya kwamba ni “itikadi hatari” na akisema kwamba wafuasi wake hawana akili ikiwa wanaamini wako kwenye “njia ya maendeleo.”  "Fikra za kijinsia, leo, ni mojawapo ya ukoloni hatari zaidi wa kiitikadi," papa alisema katika mahojiano na gazeti la La Nacion la Ajentina. “Kwa nini ni hatari? Kwa sababu inafifisha tofauti na thamani ya wanaume na wanawake.”  Papa amerudia mara kwa mara kupinga nadharia ya jinsia kwa miaka mingi, hata kama amesisitiza haja ya kuwakaribisha na kutoa huduma ya kichungaji kwa watu waliobadili jinsia.

Siku hizi talaka zimezidi - Askofu Malasusa

Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa amedai kuwa kwa sasa jamii imekosa hali ya upendo hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya mahusiano mengi kuvunjika. Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa. Askofu Malasusa amesema kauli hiyo Desemba 25, 2018  katika ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam ambapo amesema wana ndoa wengi wanahofu na mahusiano. Malasusa amesema “siku hizi talaka zimezidi jamii haina upendo wala hofu ya Mungu, hofu imejaa katika ulimwengu, wengi waliopo katika ndoa hawana hakika kama wataendelea,’’ amesema. Aidha ameongeza kuwa “malaika anasema usiogope nitawaletea habari njema, tena katika aya yetu ya siku ya leo tunasema tumepewa mtoto mwanamume, yeye yupo tayari kubadilisha mitazamo yetu kutuondoa katika hofu na kuwa wajasiri katika maisha yetu....

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte asema Mungu ni 'mpumbavu'

Duterte anafahamika kwa kutamka maneno ya kuzua ubishi Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amemwita Mungu "mpumbavu", hatua ambayo imekera sana watu katika taifa hilo lenye Wakatoliki wengi. Kiongozi huyo amesema hayo kwenye hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga. Aidha, amekosoa vikali hadithi ya Adam na Hawa kuhusu jinsi walivyotenda dhambi na kuondolewa kutoka kwenye neema ya Mungu. Kadhalika, amekosoa wazo kwamba kila binadamu tangu wakati huo huzaliwa akiwa na dhambi asilia. Bw Duterte anajulikana sana kwa matamko yake yenye kuzua utata pamoja na matusi yenye kutumia lugha kali dhidi ya wapinzani wake. ' Ingawa kanisa na raia wamemshutumu kwa hilo, afisi ya rais huyo imesema alikuwa tu anaeleza imani yake binafsi. Rais huyo amewahi kumshutumu pia Papa kwa kutumia maneneo makali na ana historia pia ya kuwatusi viongozi wengine. Tamko la sasa alilitoa katika hotuba mji wa Davao, mji ambao alikuwa kiongozi wake kabla ya kuwan...

KUYANYAMAZIA MAFUNDISHO YA UONGO NI KUYASHIRIKI

HADI hapo , nilitaka kutoa picha tu ya mafundisho tusiyoyasomea ambayo baadhi yetu wameshajiingiza katika kufundisha . Lakini , kwa nini tunafanya hivyo ? Bila shaka, sababu ni tatu : mosi , kutokujua mafundisho ya Kanisa Katoliki ni yapi ; pili , kutekwa na vyama vya kitume au vikundi vya dini visivyojali wala kujua mafundisho ya Kanisa Katoliki na tatu , ni tatizo la kumkubali bwana wa pili , ndiye pesa (Mt 6:24). Mintarafu, kutokujua mafundisho ya Kanisa Katoliki ni yapi ni aibu. Ni aibu kwa padri aliyeandaliwa kuwa mwalimu katika Kanisa kutokujua kitu. Ni aibu kuketishwa chini na kufundishwa mambo batili na kishapo kuinuka yeye mwenyewe kufundisha mambo yasiyo ya Kanisa lake. Tuseme, basi “tumeliwa akili” na wapagani, Wapentekoste, Waislamu na kadhalika. Inakuaje tuache mafundisho ya kwetu nasi tutumikie dini au makanisa mengine?  Inakuwaje sisi tulioandaliwa kuwa walimu tugeuzwe kuwa wanafunzi na wale tuliotazamiwa ku...

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho'

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho' Makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican yamesema hatua ya Papa Francis kuomba radhi kutokana na kashfa ya udhalilishaji wa kingono uliofanywa na padri na askofu Chile ni sawa na kutangaza hali ya hatari kiroho katika Kanisa la Chile.Papa amewaomba waathirika kwenda Rome ili awaombe radhi pamoja na kuwaita maaskofu wote wa Chile kwa mkutano wa dharura kujadili namna ya kurekebisha madhara yaliyotokana na kashfa hiyo ambayo imeichafua taswira ya Kanisa Katoliki nchini Chile na sifa ya Papa. Msemaji wa Vatican Grek Burke amesema waraka wa Papa kwa Kanisa Katoliki Chile ni kukiri kuwa alifanya makosa katika mtizamo kuhusu madhila waliyopitia waathiriwa. Hapo jana, Papa alikiri kuwa alifanya makosa makubwa katika maamuzi aliyoyachukua kuhusu sakata la udhalilishaji wa kingono Chile.