Kim Kardashian West anajipanga kubadilisha jina la nguo zake za ndani kufuatia shutuma kali za kudunisha mila. Raia wa Japani wanaotumia mitandao ya kijamii walishutumu vikali jina la kibiashara la nguo hizo, Kimono. Kimono ni jina la vazi la taifa na kitamaduni nchini Japani. Awali Bi Kardashian, alijitetea na kusema hatobadili jina hilo, akisema halikuwa lengo lake kukashifu vazi au utamaduni wa jamii fulani. Lakini leo Jumanne, amesema kuwa atatangaza jina lengine la nguo hizo hivi karibuni. Ruka ujumbe wa Instagram wa kimkardashian Mwisho wa ujumbe wa Instagram wa kimkardashian Nyota huyo wa Televisheni, mwanamitindo na mbunifu wa mavazi ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa: "Kila siku nasikiliza watu, najifunza na kukua… Nilipotangaza jina la nguo zangu, nilifanya hivyo nikiwa na nia njema moyoni." Kimono ni vazi rasmi nchini Japani toka Karne ya 16 Ameongeza: "Baada ya kulifikiria kwa kina, nitazizindua tena kwa jina jipya." Ki...