Mrembo Hamisa Mobetto amejizolea umaarufu mkubwa kwenye kazi yake ya mitindo na urembo, hadi sasa kwenye muziki wa Bongo Fleva. Haya ni mambo 10 ya kawaida ambao huyafahamu kuhusu mrembo huyo.
1. Sauti ya Hamisa Mobetto ndio inasikaka kwenye wimbo wa Diamond Platnumz, Lava Lava na Mbosso uitwao Jibebe. Sauti ya mwanamke inayosikika 'I like ndio ya Hamisa.
2. Kwa miaka miwili mfululizo Hamisa Mobetto ameshinda tuzo ya Starqt Awards ambazo hutolewa nchini Afrika Kusini.Mwaka 2017 alishinda kupitia kipengele cha People Choice Awards, pia aliwania kwenye kipengele cha Super Mum. Starqt Awards ni tuzo zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine.
3.Tangu akiwa mdogo Hamisa anakiri kuwa alipenda sana muziki na alitamani kuwa mwanamuziki. Kutokana na mahaba yake kwenye fedha akajikuta ameingia kwenye movie na mitindo.
4. Mashabiki wengi wanajua kuwa wimbo wa kwanza Hamisa Mobetto kurekodi ni Madam Hero kutokana ndio wa kwanza kutoka kwake, hata hivyo Hamisa alianza kurekodi wimbo uitwao Furaha.
5. Wimbo wa Hamisa, Madam Hero umeandikwa na msanii Foby na producer C 9. Utakumbuka Foby ndiye anahusika kwenye kuandika na kutunga melody za wimbo wa Dayna Nyange na Bill Nass uitwao Komela.
6. Mwaka 2010 Hamisa Mobetto alitwaa taji la Miss XXL, After School Bash. Mwaka 2011 alishiriki mashindano ya Miss Dar Indian Ocean na kushika nafasi ya pili, pia aliwahi kufanikiwa kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania.
7. Mashabiki wengi wanakumbukumbu ya Hamisa Mobetto kutokea kwenye video ya wimbo wa Diamond uitwao Salome.
Kwa mujibu wa BBC Swahili video hiyo ndio iliongozwa kutazamwa zaidi nchini Kenya kwa mwaka 2016 ikiipita video, Work ya Rihanna na Drake.
8. Kwenye wimbo wa Diamond Platnumz unaokwenda kwa jina la Nikifa Kesho, Hamisa Mobetto ndio amefanya back vocal za wimbo huo.
9. Hamisa Mobetto ni Mrembo mwingine aliyewahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania na baada ya kutoshinda kuingia kwenye Muziki wa Bongo Fleva.
Awali alifanya hivyo Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mshindi namba mbili wa Miss Tanzania mwaka 2006, huyou ameweza kufanya kazi na wasanii wakubwa kama AY.
10. Urafiki wa Hamisa Mobetto na Lira Garole ulianzia kwenye mtandao wa Instagram kwa kutumia Direct Message (DM).
Kama ulikuwa hujui Lira Garole aliwahi kuwa mpenzi wa msanii Marekani, Chris Brown, pia alionekana kwenye video ya wimbo uitwao Sorry wa Rick Ross na Chris Brown
Maoni