Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya USAGAJI

Waafrika Kusini waandamana kisa Makonda

Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake. Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini. “ Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu ”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao. Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na...