Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya The Mafik

Msanii wa The Mafik akamatwa kwa wizi

Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi. Wasanii wanaounda kundi la The Mafik, Hamadai (kushoto) Mbalamwezi (kati kati) na Rhino (kulia) Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin. Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu. Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea. East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kama...