Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ZIARA

Rais Donald Trump afanya ziara ya kushutukiza nchini Iraq

Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais wa Marekani Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq. Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa White house. Bw Trump alisema Marekani haina mpango wa kuondoka nchini Iraq. Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo. Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Iraq kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi la Islamic State. Hata hivyo mkutano uliopangwa kati ya Bw Trump na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ulifutwa. Ofisi ya Bw Mahdi ilisema hiyo ni kwa sababu ...