Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NGUVU ZA KIUME

​WANYANYUA UZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

Wanaume wanaonyanyua vitu vizito mara kwa mara wana asilimia kubwa ya kuwa rijali zaidi,  Utafiti uliofanywa na Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Harvard cha nchini Marekani  umethibitisha. Taarifa ya utafiti huo inaeleza kuwa Wanaume wenye utaratibu wa kunyanyua vitu vizito mara kwa mara au kuushughulisha mwili zaidi wana faida ya kuwa rijali kwa kuwa na mbegu nyingi za uzazi kuliko wanaume ambao kazi zao hazihitaji sana kuushughulisha mwili. Wanasayansi wa chuo hicho wamefanya utafiti huo kwa lengo la kutafuta suluhisho la tatizo la utasa linaoonekana kuwa ni mtambuka.  Pia wamegundua kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya afya ya uzazi ya Mwanaume na mazingira yake ya kikazi na mahitaji ya kimwili. Utafiti huo uliofanywa na  Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Harvard na matokeo yake  kuchapishwa  katika jarida la “Human Reproduction” ulilenga kuchunguza namna kemikali kutoka katika mazingira na mtindo wa maisha inavyoweza kuathiri afya ya uzazi kwa mwanadamu. Ulihu...