Ruka hadi kwenye maudhui makuu

​WANYANYUA UZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

Wanaume wanaonyanyua vitu vizito mara kwa mara wana asilimia kubwa ya kuwa rijali zaidi,  Utafiti uliofanywa na Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Harvard cha nchini Marekani  umethibitisha.


Taarifa ya utafiti huo inaeleza kuwa Wanaume wenye utaratibu wa kunyanyua vitu vizito mara kwa mara au kuushughulisha mwili zaidi wana faida ya kuwa rijali kwa kuwa na mbegu nyingi za uzazi kuliko wanaume ambao kazi zao hazihitaji sana kuushughulisha mwili.


Wanasayansi wa chuo hicho wamefanya utafiti huo kwa lengo la kutafuta suluhisho la tatizo la utasa linaoonekana kuwa ni mtambuka. 


Pia wamegundua kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya afya ya uzazi ya Mwanaume na mazingira yake ya kikazi na mahitaji ya kimwili.


Utafiti huo uliofanywa na  Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Harvard na matokeo yake  kuchapishwa  katika jarida la “Human Reproduction” ulilenga kuchunguza namna kemikali kutoka katika mazingira na mtindo wa maisha inavyoweza kuathiri afya ya uzazi kwa mwanadamu.


Ulihusisha Wanaume na Wanawake 1,500 ambao walikuwa wakitafuta matibabu ya afya ya uzazi , ambapo wenza 377 walikuwa wakitafuta matibabu ya utasa.


Uchunguzi wa kina ulibainisha kwamba Wanaume walioripoti kufanya shughuli nyingi za kimwili katika maeneo yao ya kazi walikuwa na asilimia 46 zaidi ya idadi ya mbegu za uzazi ikilinganishwa na wale walio na kazi chache za kuushughulisha mwili muda wa kazi na wenye  kufanya shughuli nyingi za kimwili kazini walikuwa na viwango vya juu vya homoni aina ya testosterone na kwa upande wa wanawake walikuwa na estrojeni.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...