Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.07.2019: Lindelof, Pogba, Bruce, Delph, Lukaku, Diaz, Kean Barcelona inamnyatia beki wa Manchester United na raia wa Sweden Victor Lindelof, 24, huku ikiwa beki wa Ajax Matthijs de Ligt anatarajiwa kujiunga na Juventus. (Mundo Deportivo - in Spanish) Real Madrid watalazimika kulipa dau litakalovunja rekodi la £162m kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kutoka Manchester United. (Marca) Mkufunzi wa klabu ya Sheffield Wednesday Steve Bruce ataunga mkono ofa yoyote kutoka Newcastle baada ya kupigiwa upatu kumrithi Rafael Benitez. (Chronicle) Naibu mkufunzi wa klabu ya Manchester City Mikel Arteta na mkufunzi wa Nice Patrick Vieira wameonywa kuhusu kazi ya Newvcastle na Benitez. (Sun) Everton ni miongoni mwa klabu zilizo na hamu ya kumsaini kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Fabian Delph, 29. (Sky Sports) Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutokuba...