Rais Magufuli majuzi aliwataka wananchi kuwapuuza wanaodai serikali inakopa sana Serikali ya Tanzania imesema deni la jumla la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 3 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Desemba hadi Machi mwaka huu. Serikali hiyo imepuuzilia mbali taarifa zilizochapishwa na gazeti moja nchini humo zilizodai kwamba deni la taifa hilo la Afrika Mashariki liliongezeka Sh trilioni 12 katika kipindi hicho. Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amelitaka gazeti la mwananchi "kuomba radhi kwa umma kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho Jumapili" kupitia ukurasa wa mbele wa gazeti hilo na kwenye mitandao ya kijamii. Dkt Abbas amesema baada ya gazeti hilo kusisitiza "kuwa hawana nia mbaya, serikali imezingatia utetezi huo na inawapa nafasi ya kujirekebisha zaidi". Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya Benki Kuu ya Tanzania inasema katika kipindi hicho, deni la serikali liliongezeka ...