Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tanzania yaitaka Mwananchi kuomba radhi kwa taarifa kuhusu deni la taifa


Rais Magufuli majuzi aliwataka wananchi kuwapuuza wanaodai serikali inakopa sana

Serikali ya Tanzania imesema deni la jumla la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 3 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Desemba hadi Machi mwaka huu.


Serikali hiyo imepuuzilia mbali taarifa zilizochapishwa na gazeti moja nchini humo zilizodai kwamba deni la taifa hilo la Afrika Mashariki liliongezeka Sh trilioni 12 katika kipindi hicho.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi amelitaka gazeti la mwananchi "kuomba radhi kwa umma kwa siku mbili mfululizo kuanzia kesho Jumapili" kupitia ukurasa wa mbele wa gazeti hilo na kwenye mitandao ya kijamii.


Dkt Abbas amesema baada ya gazeti hilo kusisitiza "kuwa hawana nia mbaya, serikali imezingatia utetezi huo na inawapa nafasi ya kujirekebisha zaidi".



Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya Benki Kuu ya Tanzania inasema katika kipindi hicho, deni la serikali liliongezeka kutoka shilingi trilioni 47 hadi shilingi trilioni 49 pesa za Tanzania.


"Deni hilo linajumuisha mikopo kutoka kwa nchi wahisani, mashirika ya fedha ya kimataifa pamoja na mabenki ya kibiashara ya kimataifa," taarifa hiyo inasema.


"Deni la ndani la serikali linajumuisha dhamana za serikali za muda mfupi na hati fungani za serikali pamoja na madeni mengineyo."


Serikali inasema deni la nje la sekta ya kibinafsi katika kipindi hicho cha kuanzia Desemba 2017 hadi machi 2018 lilipanda kwa shilingi tilioni moja kutoka Sh trilioni 9 hadi Sh trilioni 10.


"Kwa hivyo, deni la taifa ambalo linajumuisha deni la serikali la ndani na nje la sekta ya binafsi liliongezeka kwa Sh trilioni 3 kutoka Sh trilioni 56 mwezi Desemba 2017 hadi Sh trilioni 59 mwezi Machi 2018," taarifa hiyo ya BoT inasema.


Benki hiyo imesema ongezeko hilo lilitokana na mikopo mipya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.


Kadhalika, kutokana na malimbikizo ya riba, hasa kutoka kwa nchi za kundi lisilo la wanachama wa wa Paris ambazo hazijatoa msamaha wa madeni kulingana na makubaliano.


Benki hiyo imesema kuwa licha ya hayo, "deni la taifa bado ni himilivu".


"Kuongezeka kwa deni la taifa kunatokana na jitihada za kujenga mazingira bora zaidi ya kuongeza uzalishaji katika sekta mbalimbali za uchumi ili kufikia azma ya Tanzania ya viwanda yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025."


Tamko la benki hiyo linaonekana kukariri msimamo wa Rais wa Tanzania John Magufuli ambaye majuzi alitoa wito kwa wananchi kuwapuuza wanaodai kwamba Tanzania "inakopa sana".


Kiongozi huyo alisema mikopo inayochukuliwa na taifa hilo ina manufaa na itachochea ukuaji wa uchumi.


Wakati wa kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kiongozi huyo alieleza matumaini kwamba uchumi wa Tanzania utatengemaa.


"Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4," alisema


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...