Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump

Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia.


Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni.


Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea.


Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza, lakini sasa kumeingia shaka kuhusu hilo.


Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje Kim Kye-gwan akisema iwapo Marekani "itatubana na kusisitiza kwamba ni lazima tusalimishe bila masharti silaha zetu za nyuklia basi hatutakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itatulazimu kutafakari upya iwapo tutakubali mkutano unaotarajiwa kufanyika karibuni kati ya DPRK-US.



Korea Kaskazini kirasmi hufahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK).


Bw Kim amesema Korea Kaskazini "ilikuwa na matumaini makubwa kwamba mkutano huo ungechangia kupunguza wasiwasi katika Rasi ya Korea na kuwa hatua muhimu katika kuunda siku za usoni zenye matumaini makubwa.


"Hata hivyo, inasikitisha sana kwamba Marekani inatuchokoza kabla ya mkutano huo kwa kutoa matamko ya kushangaza."


Mapema Jumatano, dalili za wasiwasi zilianza kutokea, Korea Kaskazini ilipojiondoa kutoka kwa mazungumzo yaliyokuwa yamepangwa kati ya nchi hiyo na Korea Kusini.



Kim na Trump wanatarajiwa kukutana Singapore 12 Juni

Maafisa wa ngazi ya juu wa mataifa hayo walitarajiwa kukutana katika eneo la mpakani ambapo majeshi hayaruhusiwi kujadiliana maelezo zaidi kuhusu makubaliano ambayo yalikuwa yameafikiwa katika mkutano mkuu kati ya mataifa hayo mwezi uliopita.



Lakini Korea Kaskazini ilijiondoa ikisema imekerwa na mazoezi makubwa ya kijeshi yanayoandaliwa kati ya Korea Kusini na Marekani.


Mazoezi hayo ya kijeshi, yaliyopewa jina Max Thunder yalitarajiwa kufanyika katika kipindi ambacho michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ilikuwa inafanyika, lakini yakaahirishwa baada ya matumaini ya kuimarika kwa uhusiano kati ya Korea Kusini na Kaskazini kutokea.


Korea Kaskazini ilikuwa awali imesema ilifahami kwamba operesheni hiyo ya kijeshi ingeendelea.




Lakini KCNA wamesema sasa kwamba mazoezi hayo ya kijeshi ni "uchokozi" na maandalizi ya uvamizi, jambo linaloashiria kurejelewa kwa lugha kali iliyokuwa inatumiwa wakati wa uhasama kati ya Marekani na Korea Kusini


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...