Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAHUSIANO

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) yaipata Ukraine ukiukaji wa haki za mashoga

Kiev imeamriwa kulipa fidia kwa wanandoa kwa kukataa mara kwa mara kusajili ndoa yao ECHR inaipata Ukraine katika ukiukaji wa haki za mashoga Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) imeiamuru Ukraine kulipa fidia kwa wapenzi wa jinsia moja baada ya majaribio mengi ya kusajili ndoa yao bila mafanikio nchini humo. Mahakama ilitangaza uamuzi wake kwa kauli moja Alhamisi katika taarifa kwa vyombo vya habari. Walalamikaji wawili, Andrey Maymulakhin na Andrey Markiv, waliozaliwa mwaka wa 1969 na 1984, mtawalia, ni wanandoa wa jinsia moja kutoka Kiev. Wawili hao, ambao "wamekuwa wakiishi pamoja katika uhusiano thabiti na wa kujitolea tangu 2010," walituma maombi kwa ofisi saba za kufunga ndoa mnamo Oktoba 2014. Mashirika yote ya serikali yalikataa kusajili ndoa zao, wakitaja katiba ya Ukraine na Kanuni zake za Familia, ambayo inafafanua. ndoa kama muungano kati ya mwanamume na mwanamke. Licha ya kwamba ndoa za watu wa jinsia moja bado ni kinyume cha sheria nchini, ECHR iliona...

Utafiti: Matumizi ya simu husababisha kuwa wapenzi wengi

Utafiti: Matumizi ya simu yaliyokithiri husababisha kuwa wapenzi wengi miongoni mwa wanafunzi Matumizi ya simu yanasababisha wapenzi wengi? Katika utafiti wa zaidi ya watu 3,400 nchini Marekani wanaosoma shahada ya kwanza, wale waliosema wana matatizo na muda wanaotumia katika simu zao wanaripotiwa kuwa na wapenzi wengi pia. Na wanadhaniwa kuwa na msongo wa mawazo, mmoja wa watafiti amesema kuwa matokeo yautafiti yanashangaza. Watafiti kutoka chuo kikuu cha Chicago, Cambridge na chuo kikuu cha Minnesota wamefanya tafiti hii ya tabia za uraibu wa simu. Lengo la utafiti huu lilikua ni kutaka kujua hali ya afya ya akili ya wanafunzi na jinsi gani simu zina matokeo katika utendaji wao. Ili kujua matumizi yaliyopitiliza ya simu za mkononi, wanafunzi waliulizwa maswali mbalimbali ikiwemo yafuatayo; Rafiki zako na familia wanalalamika hukusu matumizi makubwa ya simu? Una matatizo yoyote darasani kutokana na matumizi ya simu? Unadhani muda unaotumia simu umeongezeka? ...

Diamond hatimaye hapata mpenzi mpya

Tanasha Donna Oketch: Mkenya huyu 'anayependwa' na mwanamuziki Diamond Platnumz ni nani hasa? Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz ametangaza kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba yuko katika uhusiano wa kimapenzi na Mkenya, au si uhusiano? Platnumz amepakia video kuashiria kwamba yuko kwenye mahaba na dada kwa jina Tanasha Donna Oketch. Bi Oketch, ni mtangazaji katika kituo cha redio cha NRG nchini Kenya. NRG ni miongoni mwa vituo vipya vya redio nchini Kenya ambavyo vimekuwa vikilenga kuwavutia zaidi vijana. Diamond, ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul Juma, kwenye video ya Insta Stories Jumanne aliandika kuwa: "Maskini simba yuko kwenye mapenzi…Mmwamini, yupo kwenye mapenzi." Mwanamuziki huyo kwa utani hujiita Simba au Chibu Dangote. Video inayoonyesha vivuli vya wanaoaminika kuwa yeye na Tanasha wakitembea ufukweni inaonesha ujumbe wa "I love you Tanasha" (Nakupenda Tanasha) ambayo yameandikwa mchangani. Diamond, ambay...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Tambua njia za kufuata kuleta suluhu za mifarakano katika mahusiano

Migongano na tofauti kati ya watu wawili katika mahusiano ni kitu kisichoepukika iwe ni mahusiano ya mapenzi ,mahusiano ya mzazi na mtoto na hata mahala pa kazi. Sababu za mifarakano katika mahusiano ziko wazi;kwamba watu hawa wametoka na kukulia katikla mazingira tofauti na hivyo tabia na hulka zao ni lazima zitatofautiana.  Katika hali kama hii migongano na kutoelewana wakati mwingine ni vitu ambavyo vinatokea na kunahitajika busara na mbinu mahususi za kukabiliana na tatizo hili  Njia 7 Muhimu za Kutatua Mifarakano Katika Mahusiano   1. Kuwa wa Kwanza Kuchukua Hatua   Kunapotokea kufarakana kati ya watu wawili kwa kawaida mawasiliano huvunjika au kuwa magumu na mabaya. Kila mmoja anaweza akwa na kinyongo na mwingine. Kwa wapenzi hali hii inaweza ikawa ya kuumiza zaidi kwani inahusisha hisia kwa kiasi kikubwa;ni jukumu lako wewe kufunja ukimya na kuwa wakwanza kuleta suluhu.  Tafuta nafasi na omba kujadili na kuongea kuhusu tofauti zenu.  2. An...

Namna ya kuachana kwa amani na mpenzi wako

MAPENZI Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:  1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya:  Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya ku...

Kuna changamoto na athari kubwa sana ukioa mwanamke mzuri

AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana.  Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi.  Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine.  Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mamb...

Fahamu mambo yanayochangia kupoteza hisia za mapenzi

Lipo jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aliye kwenye uhusiano ikiwa anataka kutosheka na penzi la mpenzi wake.  Kwanza ni lazima uitosheleze akili yako, lakini pili, unapaswa kuamini kwamba uliyenaye ni bora na hata ikiwa kuna kasoro, jambo la msingi ni kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.  Anachanganya mambo, hatosheki   Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.  Lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani, ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo hilo kuliko sasa.  Hata hivyo, wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri, kama wangekuwa nao hadi leo, huenda wasingeweza kuendelea kuwa imara.  Hii ni kwa sababu, watu wengi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.  Zi...