Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kuna changamoto na athari kubwa sana ukioa mwanamke mzuri





AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana. 

Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi. 

Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine. 

Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mambo hayo. 

Aidha, wanaume wengine watakuambia hawataki kuoa wanawake wanaokunywa pombe, wanaoendekeza mambo ya anasa. Wanataka wanawake wa kutulia nyumbani, wanaomjua Mungu. Huo ni utofauti mdogo tu kwa baadhi ya wanaume wanapochagua wanawake wa kuingia nao kwenye ndoa. 

Hata hivyo, hili suala la kutaka kuoa mwanamke mzuri huwa lina tofauti ya aina yake. Mwanamke ambaye wewe unaweza kuona ā€˜umengā€™oa kifaaā€™ wenzako wanaweza kukuponda kwa kusema umependa demu asiye na hadhi yako. Ukweli uko hivyo kwamba, kibaya kwako ni kizuri kwa mwenzio. 

Nigeukie sasa kwenye kile nilichodhamiria kukizungumzia leo. Ni kuhusu athari ambazo mwanaume anaweza kuzipata endapo ataoa mwanamke mzuri kwa sura na umbo, mwenye pesa lakini limbukeni. Hapa namaanisha kwamba, wapo ambao ni wazuri, waliokwenda shule, wenye kazi zao ila wanapoingia kwenye maisha ya ndoa, wanawaheshimu waume zao kupita maelezo. Yaani vipato vyao, elimu na mali zao havina thamani mbele ya mume. 

Ukibahatika kuoa mwanamke wa sampuli hii utayafurahia maisha. Lakini ukioa aliyejaaliwa vitu hivyo kisha akawa si muelewa wala hajui thamani ya mume na ndoa, andika maumivu. Kimsingi zipo athari nyingi za kuoa mwanamke mwenye pesa, mzuri kwa muonekano, ā€˜aliyebukuaā€™ sana lakini akawa limbukeni. Leo nitagusia tatu. 

Kusalitiwa kuko nje nje 

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi malimbukeni ambao wanajijua ni wazuri na wana pesa zao wakiudhiwa kidogo tu ni wepesi kuchepuka hata kwa kuwashawishi wanaume wengine kwa pesa. Utakuta mume kamkosea kidogo au kamkera bila kudhamiria lakini yeye anaona njia sahihi ni kutorudi nyumbani. Anaweza kwenda kulala hotelini mpaka pale mume atakapomfuata na kumpigia magoti. Wapo wanawake wa hivyo! 

Ni wepesi kuomba muachane 

Ukifuatilia sana wanawake wenye vigezo hivyo wanajiamini sana, hawa ndiyo wanaoongoza kwa kuomba talaka. Kosa dogo tu, atakuambia kama vipi muachane. 

Anasema hivyo akijua wapo wanaume wengi wanaomsumbua na hatapungikiwa lolote. Tena hali inaweza kuwa mbaya sana kama wakati huo hamjajaaliwa mtoto kwani atajua hatakosa kitu akikuacha. Pesa anayo, ana uhakika wa kupata mwanaume mwingine fasta, kwa hiyo anaona hana cha kupoteza au kukikosa akikutosa. 

Rahisi kukutawala 

Chunguza sana utabaini kuwa, wanaume ambao wanasumbuliwa na wake zao wana vigezo hivyo. Baadhi ya wanawake wenye pesa na wanajijua ni wazuri wanapenda sana kuonekana wao ndiyo wenye sauti ndani ya nyumba. Watakataa kuelekezwa wala kupewa amri na wanaume zao hata kwenye masuala ya msingi. Hawa ndiyo wale ambao wanataka kurudi nyumbani muda wowote wanaotaka na wasiulizwe. 

Watataka wawe wenye maamuzi ya mwisho na kila jambo la kifamilia washirikishwe laa sivyo kinanuka. Hili ni tatizo! Kimsingi ninachotaka kukifikisha kwa wanawake ni kwamba, ndoa ni heshima. Ukijaaliwa kupata mwanaume wa kukuingiza ndani, jitahidi kuithamini ndoa yako. Jua wapo wanawake wenye kila kitu lakini wamekosa wanaume wa kuwaoa na wanaitamani heshima ya ndoa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...