Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Vigogo Kampuni ya Acacia kortini kwa tuhuma za rushwa




Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo. 

Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatano Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007. 

Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania Oā€™mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara. 

Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wakati wa upimaji wa ardhi kwa ajili ya kupanua eneo la mgodi huo. 

Vile vile mnamo Machi 7, 2012, Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali, Joseph Thomas Kleruu alipewa tenda ya kufanya tathmini ya shamba Na. 190 lililopo mkoani humo kinyume cha sheria ili kuwasaidia kupata eneo la kupanua mgodi huo. 

Imeelezwa kuwa kati ya Januari 2013 na Disemba 2017, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakunguru, Abel Mnyakibari alipewa rushwa ya jumla ya shilingi 966,687,343 kutoka katika mgodi huo ili ajiepushe na kukataa kuwalipa fidia baadhi ya wanakijiji vile vile kati ya Januari 2010 na Disemba 2015, Mwenyekiti huyo alipewa rushwa ya jumla ya shilingi 90,251,475 kwa ajili ya kumshawishi asifatilie fidia ya wanakijiji zaidi ya 800 wa Kijii cha Kewanja. 

Kati ya Januari 2006 hadi Mei 2018, Diwani wa Kata ya Kemambo na Mkurugenzi Mtendaji, Bogomba Chichake na Tanzania O'mtima walipewa zabuni ya shilingi 7,709,575,914,19 na shilingi 1,102,880,8 ili kutoihamisha shule ya Nyabigena kutoka eneo la Mrambwe kwenda eneo la Mgema kwa ajili ya kuusaidia mgodi huo kujenga shule kwa bei nafuu. 

Kampuni ya Acacia inamiliki migodi mitatu ya dhahabu nchini ikiwemo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi, imeandikishwa katika soko la hisa la London. Mnamo Julai 2017, Kampuni hiyo iliipeleka Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi kuhusiana na katazo la kusafirisha makinikia

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...