Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAKINIKIA

Vigogo Kampuni ya Acacia kortini kwa tuhuma za rushwa

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, kupitia kampuni yake ya North Mara Gold Mine iliyopo mkoani Mara, imeingia katika kashfa baada ya Maafisa Waandamizi wa kampuni hiyo wawili kushtakiwa kwa tuhuma za rushwa ili kupata upendeleo dhidi ya maslahi ya wanavijiji na Serikali ya mkoa huo.  Washtakiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Tarime siku ya Jumatano Oktoba 10, 2018 na kusomewa mashtaka ya rushwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.  Kwa nyakati tofauti, watuhumiwa Marteen Van Der, Johannes Jensen, Joseph Kleruu, Bomboga Chikachake, Tanzania O’mtima na Abel Kinyimari wameshtakiwa kwa utoaji na upokeaji wa rushwa wa namna mbalimbali kwa Maafisa wa Serikali na wanasiasa wa mkoani Mara.  Mei 17, 2013 watuhumiwa Marteen Van Der na Johannes Jensen walitoa rushwa ya jumla ya shilingi 93,896,000 kwa Mthamini Mkuu wa Ardhi wa Serikali Adam Yusuph pamoja na kumpa Peter Mrema 30,000,000 ili kupata upendeleo wak...

Hongera MAGUFULI: Barrick Gold kuilipa Tanzania dola milioni 300 za kimarekani sawa billion 700 za kitanzania

MTEULE THE BEST Barrick Gold kuilipa Tanzania dola milioni 300 za kimarekani Kampuni ya inayomiliki migodi ya madini nchini Tanzania, Barrick Gold imekubali kuilipa Serikali ya Tanzania hisa ya asilimia 16 na mgawo wa asilimia hamsini ya mapato ya mauzo ya dhahabu kutoka migodi 3 inayoimiliki. Hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya za madini ya Tanzania baada ya kampuni hiyo kukubali kuwa na mazungumzo na Serikali ya Tanzania . Vilevile kampuni hiyo imekubali kutoa Dola za Kimarekani milioni 300 kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kutokana na biashara ya kampuni hiyo. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Prof. Thornton amesema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa. Kampuni ya dhahabu kujadiliana na Tanzania kuhusu malipo Tanzania yapoteza matrilioni ya pesa za madini Mambo muhimu kuhusu sakata ya madini Tanzania Kwa upande wake...