Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NDEGE VITA

KWANINI RUBANI WA NDEGE ZA KIVITA AKIOKOKA KWENYE AJALI YA NDEGE HAWEZI TENA KURUSHA NDEGE

Picha
Tangu mwishoni mwa miaka ya 1940, maelfu ya marubani wa kivita wamenusurika kwenye ajali mbaya kutokana na matumizi ya viti vya kisasa vya kutoroka nje ya ndege "Ejection Seat" Kutoroka huko kunahusisha kuuweka mwili wa binadamu katika nguvu za uvutano (G-Force) zinazofikia 12-14 Gs ndani ya sekunde, na kusababisha mkandamizo wa uti wa mgongo, kuvunjika pingili, au uharibifu wa muda mrefu wa 'musculoskeletal'. Kila utorokaji huja kwa gharama kubwa ya afya na kikazi, huku marubani wengi ambao hujifyatua nje zaidi ya mara moja hawarejei kwenye majukumu ya mstari wa mbele wa kuruka. Kujifyatua au kutoroka nje ya ndege zoezi la vurugu kwa asili yake ya kimuundo, na hutumia chaji za vilipuzi au roketi kulipua kiti na rubani kurushwa nje ya ndege kwa sekunde. Mkandamizo wa juu unaweza kufikia 20 Gs (Hii ni mara 20 ya uzito wa mwili wako) ambapo hukandamiza mgongo na kuumiza mwili. Marubani mara nyingi hupata nyufa ya uti wa mgongo, majeraha ya shingo, au majeraha ya tishu l...