Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 21, 2018

Bilioni 20 za Mo kwa Simba zapangiwa matumizi

Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba. Mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba Swed Mkwabi, ameweka wazi mipango yake na kuomba wanachama wa klabu hiyo wamchague.  Kampeni za uchaguzi huo wa Simba utakaofanyika November 4, 2018, zimefunguliwa rasmi jana, na leo Mkwabi ameweka wazi mipango yake kwa kusema atahakikisha pesa ya uwekezaji bilioni 20 itakayotolewa na Mohammed Dewji inaongezeka maradufu.  ''Bilioni 20 ni pesa nyingi lakini inahitaji weledi mkubwa wa kuifanya endelevu, inaweza ikachotwa ndani ya miaka mitatu ikaisha tukashindwa kuzalisha tena tukarudi tulikotoka kwa hiyo kama nitapata fursa kwa kushirikiana na wenzangu tutatengeneza misingi ya kibiashara kuitoa katika bilioni 20 kuifanya iwe zaidi'', ameeleza.  Aidha Mkwabi amesema kuwa ameshagundua wanachama wa Simba wanataka wajumbe wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa ajili ya Simba na anaamini wanajua kuchuja mjumbe gani anafaa na yupi hafai hivyo hat...

Namna ya kuachana kwa amani na mpenzi wako

MAPENZI Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:  1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya:  Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya ku...

Daraja refu zaidi duniani

mteulethebest Daraja refu zaidi duniani linalounganisha Hong Kong-Zhuhai China litafunguliwa rasmi hapo kesho. Daraja hilo lenye umbali wa kilomita 55km  limegharimu takriban dola bilioni $20 za Marekani. Ujenzi  ulianza mwaka wa 2009. Safari ya kawaida kati ya China na Hong Kong ilikuwa inachukua muda wa takriban saa 4. Daraja hili linapunguza muda huo wa usafiri hadi dakika 30 pekee. Je nini kinaizuia Afrika isipige hatua ya maendeleo  kama hii?

Mo Dewji Atoa neno kwa mara ya kwanza

Mo Dewji afunguka kwa mara ya kwanza Mfanyabishara Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ametoa neno la shukrani kwa mwenyezi Mungu na watanzania kwa kumuombea katika kipindi chote alichokuwa mateka.  Jumatatu hii Mo ambaye pia ni mwekezaji wa klabu ya Simba, ametweet kwa mara ya kwanza kuwashukuru watanzania ambao walikuwa wanamuombea katika kipindi chote kigumu alichopitia.  “Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima,” alitweet Mo jioni ya leo.  Mfanyabishara huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akielekea mazoezini na kuachiwa Alfajiri ya Oktoba 19, ambapo alikutwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana.

Injinia Alphonse Augustino Cherehani: Asimulia vipi alivyopatikana hai siku 3 baada ya kuzama MV Nyerere?

Jina la Injinia Augustine Cherehani lilianza kuvuma katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania siku tatu baada ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake katika ziwa Victoria kati ya kisiwa cha Ukerewe na Ukara. Injinia Augustine Cherehani katika kile kilichowaacha wengi vinywa wazi aliokolewa wakati tumaini la kupata walio hai likiwa limesha malizika. Injinia ambaye ndiye fundi mkuu wa kivuko hicho kilichopinduka Mwezi wa tisa tarehe 20 mwaka wa 2018 na kuua watu zaidi ya 225, alimsimulia mwandishi wa BBC Eagan Salla mkasa mzima. 'Siku kama siku nyingine' Siku ya tukio Injinia anasema ilkuwa siku kama siku nyingine lakini kwao kwa misingi ya usafirishaji ilikuwa siku ya kazi kubwa kwani ilikuwa ni siku ya gulio eneo la Bugorora. Kawaida wakazi wa kisiwa cha Ukara hufurika gulioni kujipatia mahitaji mbalimbali na siku hiyo ilikuwa vivyo hivyo. Kabla ya safari kama kawaida alikagua chombo (MV Nyerere) zikiwemo Injini zake ...

TFF yafanya mabadiliko haya, yamteua Ammy Ninje

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Ammy Ninje. Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Jumamosi Oktoba 20, 2018 Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala ilipitia masuala mbalimbali ikiwemo kumthibitisha Ammy Ninje katika nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.  Nafasi hiyo ilikuwa inakaimiwa na Oscar Milambo ambaye ataendelea na jukumu lake la Ofisa Maendeleo wa Vijana. Pia Kamati hiyo ya Utendaji imepitisha tarehe ya Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka ambao utafanyika Jijini Arusha Disemba 29, 2018.  Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na umepata siku 60 za kutangazwa kabla ya kufanyika.  Aidha kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimepitisha mabadiliko madogo kwenye kamati ndogo ndogo za TFF. Mabadiliko hayo yametokana na baadhi ya Wajumbe kujiuzulu na wengine kukabiliwa na majukumu mengi.  KAMATI YA NIDHAMU   1. Kiomoni  Kibamba  - Mwenyekiti  2. Peter Hella - M/Mkiti  3. Kassim Dau  - Mjum...