Mo Dewji afunguka kwa mara ya kwanza
Mfanyabishara Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ametoa neno la shukrani kwa mwenyezi Mungu na watanzania kwa kumuombea katika kipindi chote alichokuwa mateka.
Jumatatu hii Mo ambaye pia ni mwekezaji wa klabu ya Simba, ametweet kwa mara ya kwanza kuwashukuru watanzania ambao walikuwa wanamuombea katika kipindi chote kigumu alichopitia.
“Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yangu. Pamoja na kupitia kipindi kigumu lakini daima amesimama upande wangu. Marafiki zangu, napenda kuwashukuru wote kwa maombi yenu na kunitakia kheri. Mungu awazidishie kwa wema wenu. Baraka za Mungu ziwe nanyi leo na daima,” alitweet Mo jioni ya leo.
Mfanyabishara huyo alitekwa na watu wasiojulikana Alfajiri ya Oktoba 11, wakati akielekea mazoezini na kuachiwa Alfajiri ya Oktoba 19, ambapo alikutwa ametelekezwa katika viwanja vya Gymkana.
Maoni