Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Pembe ya Afrika

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Idai yaongezeka kwa kasi nchini Msumbiji

Wafanyakazi wa shirika la uokoaji wakiwa wanajiandaa kuondoa miili kutoka kwenye helikopter Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Idai kilichoikumba eneo la kusini mwa Afrika zaidi ya juma moja lililopita,imeongezeka kwa kasi siku ya Jumamosi. Idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 242 mpaka 417,waziri wa ardhi na mazingira nchini humo Celso Correia ameeleza. Idadi hii mpya inafanya waliopoteza maisha Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kufikia 700. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi. Kimbunga kimeua takribani watu 259 nchini Zimbabwe na Malawi 56.Watu walipoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko. Lakini Umoja wa mataifa limesema maafisa wataweza kutathimini madhara pale maji yatakapopungua. Maelfu ya watu wakiwa wanasubiri kuokolewa kutoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kusini mwa Afrika Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinaadamu, OCHA imesema kuwa mto wa Buzi na ...

Rajoelina atangazwa mshindi uchaguzi wa Madagascar

Kiongozi wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa taifa hilo la kisiwa cha bahari ya Hindi katika matokeo ya awali yaliotangazwa na tume ya uchaguzi Alhamisi. Rajoelina alikuwepo wakati tume ya uchaguzi ikitangaza kwamba amepata asilimia 55.66 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 44.34 ya mshindani wake Marc Ravalomanana - ambaye hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo. Ravalomanana, ambaye pia ni rais wa zamani, amekosoa uchaguzi katika kisiwa hicho kilichoko nje ya pwani ya Afrika kwa kile alichokiita udanganyifu mkubwa. Mahakama ya katiba hivi sasa ina muda wa siku tisa kutangaza matokeo ya mwisho. Siasa nchini Madagascar, ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa na mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, kwa muda mrefu zimekuwa zikizongwa na mapinduzi ya mara kwa mara na machafuko. Rajoelina na Ravalomamana wana historia ya uhusiano mgumu kati yao, baada ya Rajoelina kuchukuwa nafasi ya Ravalomana kama akiongozi wa taifa kufuati...

Boeing 787-8 Dreamliner: Mambo matano makuu aliyoyasema Magufuli kuhusu ndege mpya ya Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli Jumapili aliongoza taifa hilo kupokea ndege mpya ya kisasa ambayo imenunuliwa kwa ajili ya kutumiwa na shirika la ndege la taifa hilo. Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ilinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL). Bei ya ndege hiyo inakadiriwa kuwa $224.6 milioni (Sh512 bilioni za Tanzania) kwa mujibu wa taarifa kwenye tovuti ya kampuni ya Boeing. Ndege hiyo iliwasili majira ya saa 11:10 jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kisha kupewa heshima ya kumwagiwa maji na baadaye Rais Magufuli akiwa na viongozi wakuu walioambatana naye akaizindua rasmi. Aidha, yeye na Makamu wake Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, waliikagua kwa kuingia ndani ya ndege ili kujionea mandhari ya ndani. Mataifa ya Afrika yaliyo na Dreamliner Ethiopia (Ethiopian Airlines )*- 19 Kenya (Kenya Airways) - 8 Morocco ...

Mazungumzo ya amani kati ya Ethiopia na Eritrea

Ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Eritrea unatarajiwa kuwasili katika nchi jirani ya Ethiopia kwa mazungumzo kuhusu juhudi za amani na kufufua matumaini ya kumalizika ugonvi uliodumu muda mrefu kabisa barani Afrika. Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema mapema mwezi huu yuko tayari kutekeleza masharti yote ya makubaliano ya amani  ya mwaka 1998-2000 yaliyomaliza ugonvi wa nchi hizo mbili, akiashiria uwezekano wa kupatiwa ufumbuzi mvutano kuhusu mpaka wa nchi hizo mbili. Rais Isaias Afwerki wa Eritrea akasema wiki iliyopita, anakaribisha kile alichokiita "risala za maana" kutoka Ethiopia na kuamua kutuma ujumbe wa kwanza rasmi wa serikali yake kuwahi kwenda Addis Abeba baada ya kupita miongo miwili . Ujumbe wa Eritrea unawaleta pamoja mshauri wa rais Yemane Gebreab, waziri wa mambo ya nchi za nje Osman Saleh na mwakilishi wa Eritrea katika Umoja wa Afrika-hayo ni kwa mujibu wa kituo cha matangazo kinachomilikiwa na serikali nchini Ethiopia. Wanajeshi ...