Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TUME YA UCHAGUZI

Rajoelina atangazwa mshindi uchaguzi wa Madagascar

Kiongozi wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa taifa hilo la kisiwa cha bahari ya Hindi katika matokeo ya awali yaliotangazwa na tume ya uchaguzi Alhamisi. Rajoelina alikuwepo wakati tume ya uchaguzi ikitangaza kwamba amepata asilimia 55.66 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 44.34 ya mshindani wake Marc Ravalomanana - ambaye hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo. Ravalomanana, ambaye pia ni rais wa zamani, amekosoa uchaguzi katika kisiwa hicho kilichoko nje ya pwani ya Afrika kwa kile alichokiita udanganyifu mkubwa. Mahakama ya katiba hivi sasa ina muda wa siku tisa kutangaza matokeo ya mwisho. Siasa nchini Madagascar, ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa na mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani, kwa muda mrefu zimekuwa zikizongwa na mapinduzi ya mara kwa mara na machafuko. Rajoelina na Ravalomamana wana historia ya uhusiano mgumu kati yao, baada ya Rajoelina kuchukuwa nafasi ya Ravalomana kama akiongozi wa taifa kufuati...

Moto wateketeza ghala la tume ya Uchaguzi

Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza ghala la tume ya uchaguzi nchini Congo. Sehemu ya Ghala lililoteketea, kwa moto. Inasemekana kuwa Mashine zaidi ya 7000 za kura na vifaa vingine vilikuwemo kwenye ghala hilo la Kinshasa ikiwa ni masaa kadhaa tangu Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) ilipotangaza kupokea vifaa mbalimbali vya uchaguzi ikiwemo mashine za kupigia kura. Kampeni za kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinaendelea baada ya kuanza rasmi Novemba 22, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 23 mwezi Desemba. Tume hiyo ya Uchaguzi ilisema kuwa imeorodhesha wapiga kura milioni 40 wanaotarajia kushiriki uchaguzi huo katika vituo vya kupigia kura 80,000 ambavyo vitakuwa na 'mashine za kupigia kura" zaidi ya 100,000. Kampeni zinaendelea wakati huu, kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura, pamoja na changamoto za kiusalama, mashariki mwa nchi hiyo. Wanasiasa wa upinzani, akiwemo mmoja wa wagombea w...