Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Baba Mtakatifu

Kujikabidhi kwa Yule anayeongoza Kanisa

Picha
2025.05.08 Uchaguzi wa Papa wa ROma.  (@Vatican Media) Mwariri mkuu wa Baraza la kipapa la Mawasiliano kwa mtazamo wa kuchaguliwa kwa Papa mpya ambaye amebainisha:“Leo hii ulimwengu uko katikati ya dhoruba,inayotikiswa na vita na jeuri.Tuombe amani.Tuombe pamoja na Petro na Petro ambaye leo hii alichukua jina la Leo,akiungana tena na Papa wa Waraka wa kitume wa “Rerum novarum.” Andrea Tornielli Jimbo la Roma lina Askofu wake, Kanisa la ulimwengu wote lina mchungaji wake. Kwa kasi ambayo inaweza  kuwashangaza tu wale wanaosoma maisha ya Kanisa kupitia lenzi za siasa, Mkutano Mkuu umemteua Mrithi wa Petro. Asante, Baba Mtakatifu, kwa kukubali. Asante kwa kusema "ndiyo" na kwa kujiacha kwa Yeye anayeongoza Kanisa. Maneno ya kukumbukwa yaliyosemwa na Paulo VI mbele ya wanafunzi wa Chuo cha Lombardia , mnamo Desemba 1968, wakati wa kipindi kigumu cha kupinga katika kipindi cha baada ya mtaguso, yanakumbuka tena: “Wengi - alisema Papa - wanatarajia kutoka kwa Papa ishara za hisia, ...

Uchaguzi wa Papa,kutoka kwa moshi mweupe hadi Habemus Papam”

Picha
2025.05.08 Papa mpya   (@Vatican Media) Hiki ndicho kilichotokea katika Kikanisa cha Sistine dakika chache ambazo zilifuatiwa na moshi mweupe,ambao unatokea kabla ya tangazo kuu la Kardinali shemasi Mamberti,akiwa katikati ya Dirisha la Baraka la Basilika ya Mtakatifu Petro kwa jina jipya la Askofu wa Roma. Na Alessandro Di Bussolo na Angella Rwezaula – Vatican. Moshi mweupe ulitokea katika bomba lililounganishwa katika Kikanisa cha Sistine, ambao umeashiria kutangaziwa waamini na ulimwengu mzima kuwa amechaguliwa Askofu mpya wa Roma, mfuasi wa Petro. Lakini je ni kitu gani kilitokea chini ya picha za msanii Michelangelo, dakika chache kabla, na ni kitu gani kitaendelea hadi kutangazwa kwa jina jipya la Papa, litakalotangazwa baada ya neno la: "Habemus Papam” yaani "Tunaye Papa" kupitia katikati ya dirisha la Baraka la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Kardinali, Shemasi wa ufaransa, Dominique Mamberti? Jina linalosubiriwa kwa hamu kubwa. Moshi mweupe   (@Vatican Media) I...