Kujikabidhi kwa Yule anayeongoza Kanisa
Andrea Tornielli
Jimbo la Roma lina Askofu wake, Kanisa la ulimwengu wote lina mchungaji wake. Kwa kasi ambayo inaweza kuwashangaza tu wale wanaosoma maisha ya Kanisa kupitia lenzi za siasa, Mkutano Mkuu umemteua Mrithi wa Petro. Asante, Baba Mtakatifu, kwa kukubali. Asante kwa kusema "ndiyo" na kwa kujiacha kwa Yeye anayeongoza Kanisa.
Maneno ya kukumbukwa yaliyosemwa na Paulo VI mbele ya wanafunzi wa Chuo cha Lombardia , mnamo Desemba 1968, wakati wa kipindi kigumu cha kupinga katika kipindi cha baada ya mtaguso, yanakumbuka tena: “Wengi - alisema Papa - wanatarajia kutoka kwa Papa ishara za hisia, uingiliaji wa nguvu na wa maamuzi. Papa haamini kwamba anapaswa kufuata mkondo mwingine wowote zaidi ya ule wa kumtumaini Yesu Kristo, anayejali zaidi Kanisa lake kuliko mtu mwingine yeyote. Yeye ndiye atakayetuliza dhoruba. Je! Ni mara ngapi Mwalimu alirudia: “Confidite in Deum. Creditis in Deum, et in me credite!”. “Muamini Mungu. Niamini hata mimi”
Papa atakuwa wa kwanza kutekeleza agizo hili la Bwana na kujiacha mwenyewe, bila uchungu au wasiwasi usiofaa, kwa mchezo wa fumbo la kutokuonekana laki kwa msaada wa Yesu kwa Kanisa lake. Sio kungojea tasa au uvivu: bali ni kungojea kwa macho katika maombi. Hii ndiyo hali ambayo Yesu mwenyewe ametuchagulia, ili aweze kufanya kazi kwa ukamilifu. Papa pia anahitaji kusaidiwa kwa maombi.”
Leo hii ulimwengu uko katikati ya dhoruba, inayotikiswa na vita na jeuri. Tuombe amani. Tuombe pamoja na Petro na Petro ambaye leo hii alichukua jina la Leo, akiungana tena na Papa wa Waraka wa kitume wa “Rerum novarum,"(unahusu “Haki na Wajibu wa Mtaji na Kazi.” Ni Waraka ulitolewa na Papa Leo XIII tarehe 15 Mei 1891.) Na kwa kuthibitishwa naye kwa imani, tujifunze pia kujiachia kwake yeye anayetawala kutoka katik mti wa msalaba, akijitwika mwenyewe majeraha ya wanadamu.
Maoni